Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
TAMWA inaungana na Watanzania wote kuomboleza msiba mkubwa wa Taifa, kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin William Mkapa, nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam.
Katika utawala wake, Hayati Mkapa alifanya mengi ikiwemo kusimamia usawa wa jinsia hasa sheria ya makosa ya kujamiiana SOSPA ya mwaka 1998, na pia aliipokea ripoti ya Beijin ambayo ilijikita katika kuleta mabadiliko kuhusu usawa wa kijinsia na kuonyesha mtazamo chanya.
Pia TAMWA itaendelea kumkumbuka Hayati Mkapa kwa kuwa wakati chama hicho kinaanzishwa mwaka 1987, Mkapa ndiye alikuwa Waziri wa Habari na alifungua mlango kwa wanahabari wanawake kuvuka kutoka hatua moja kwenda nyingine.
TAMWA tunamuombea pumziko la amani na daima tutaenzi Mchango wake.
More Stories
Majaliwa:Serikali imejipanga kukamilisha maandalizi michuano CHAN,AFCON
Uwekezaji ufanyike maporomoko ya maji Kalambo
Bunge lapitisha muswada wa Sheria za kazi,wanaojifungua watoto njiti waongezwa likizo ya uzazi