Na Dotto Mwaibale, TimesMajira Online,Iramba.
MWENGE wa Uhuru ambao umemaliza mbio zake za kukagua miradi ya maendeleo wilayani Iramba mkoani Singida leo na kukabidhiwa Wilaya ya Mkalama umeridhishwa na miradi yote huku Mkuu wa wilaya hiyo akimwagiwa sifa.
Baadhi ya miradi iliyopitishwa ni mradi mkubwa wa maji uliopo katika Kijiji cha Kyalosangi Kata ya Kinampanda ambao ulizinduliwa na Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Luteni Josephine Mwambashi ambaye aliongozana na Mkuu wa wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda na viongozi wengine.
Mradi huo mkubwa wenye tanki la lita 50,000 kwenye mnara wa mita 6, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 5 umegharimu Sh. Milioni 150, 589, 732.72 na umeongeza upatikanaji wa maji kwa asilimia 1.98 na kufikia asilimia 61 wilayani Iramba.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Luteni Josephine Mwambashi ametembelea pia chanzo cha mradi huo na kuridhishwa na mradi huo na kuufungua “Tumeona kuna kisima na tumepanda kwenye tanki tumeshuhudia kuna maji, tumeona pia nyaraka ziko vizuri na tumeona mabomba na vituo vya kuchotea maji na wananchi wanapata huduma ya maji hivyo nauzindua mradi huu na sasa nakata utepe ” amesema Mwambashi.
Mwambashi amempongeza Mkuu wa Wilaya hiyo Suleiman Mwenda kwa kusimamia vizuri fedha za Serikali katika kutekeleza miradi hiyo yote yenye manufaa makubwa kwa wananchi.
More Stories
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi
Rais Samia apongezwa kwa kuboresha huduma kwa wazee
Watu 5,000 kuhudhuria tamasha la utamaduni Songea