May 4, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwalimu ashinda Mazda CX5 kampeni mwaka umenyooka

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MWALIMU wa Shule ya Sekondari Hai mkkoani Kilimanjaro, Geofrey Pascal Paul ameibuka mshindi wa gari aina ya Mazda CX5 kupitia kampeni ya “Mwaka Umenyooka” inayoratibiwa na My Airtel App, na hivyo kubadilisha kwa kiasi kubwa maisha yake ya kila siku.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa gari hilo iliyoandaliwa na Airtel Tanzania, Mwalimu Paul amesema ushindi huo ni hatua kubwa kwake, hasa katika kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake ya kikazi.

Ameeleza kuwa awali alikuwa akitegemea usafiri wa pikipiki kwenda na kurudi shule, hali iliyokuwa ikimpa changamoto hasa nyakati za mvua, lakini sasa ana uhakika wa usafiri salama na wa uhakika zaidi.

Amefafanua kuwa hakutarajia kabisa kupata ushindi huo, kwani aliingia kwenye droo hiyo bila kujua baada ya kufanya muamala wa kawaida kupitia Airtel Money App.

Alituma shilingi 100,000 kwa ajili ya matibabu ya baba yake, jambo lililomuingiza moja kwa moja kwenye droo ya kampeni hiyo.

“Sikuwahi kufikiria kuwa siku moja ningeweza kumiliki gari la kisasa kama hili. Kwangu hii ni kama ndoto. Mungu ameniona kupitia My Airtel App.

“Nilifanya muamala wa laki moja tu kwa ajili ya kusaidia mgonjwa, lakini umeleta baraka kubwa. Ninamshukuru sana Airtel kwa kuwajali wateja wao,” amesema Mwalimu Paul kwa furaha.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Airtel Money wa Airtel Tanzania, Andrew Rugamba, amesema kampeni hiyo inalenga kurudisha kwa jamii pamoja na kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidigitali.

Ameongeza kuwa, kupitia Airtel Money App, Watanzania wanaweza kufanya miamala mbalimbali kwa urahisi zaidi huku wakichangia kukuza uchumi wa kidigitali nchini.