Na Esther Macha, Timesmajira Online,Mbeya
MWILI wa aliyekuwa mwalimu wa shule ya msingi Mbugani wilayani Chunya mkoani Mbeya,Herieth Lupembe(37),umesafirishwa kwenda mkoani lringa kwa ajili ya maziko huku lvon Tatizo Haonga(15)mwanafunzi kidato cha kwanza sekondari ya lsenyela umesafirishwa kwenda Ihanda Mbozi mkoani Songwe.
Marehemu hao walipoteza maisha mara baada ya kushambuliwa na vitu butu kichwani na watu wasiojulikana Machi 31, 2024 majira ya saa 2:30 usiku wakati Mwalimu huyo akiwa nyumbani kwake na Ivon pamoja na Haris Barnaba Mtweve (06) Mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Ken Gold aliyejeruhiwa kwa kupigwa kitu butu kichwani tukio ambalo lilithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga Machi 1, mwaka huu.
Akizungumza Machi 2,2024 Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbugani, Gideon Kinyamagoha amesema kuwa tukio hilo limeleta simanzi katika Kijiji hicho na kuwa taratibu za uchunguzi zimekamilika imekabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi.
Baba mzazi wa mwanafunzi aliyeuawa, Fackson Simchimba amesema mwili utapelekwa nyumbani kwao Mbozi mkoa wa Songwe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ,Bosco Mwanginde ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mbugani amesikitishwa na tukio hilo la kinyama hasa ikizingatiwa shule nyingi zina uhaba wa walimu.
“Hili tukio limetutia simanzi na hata wananchi wa hapa kijijini nikiwemo mimi ambaye ni Diwani wa Kata hii ya Mbugani ,tunaviachia vyombo vya ulinzi na usalama kushughulikia hili jambo,”amesema Mwanginde.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi