April 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Mpwapwa ikiwa na uongozi wa TANROAD mkoa wa Dodoma akiangalia uvunjifu wa Daraja la Tanesco

Mvua yazidi kuigawa Mpwapwa

Na Stephen Noel-Mpwapwa.

Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha kote nchini zimeendelea kuathiri miundo mbinu ya barabara na madaraja ambapo Kwa sasa daraja ambalo liko karibu na ofisi za umeme Tanesco kusombwa na maji na kupelekea mji huo kuendelea kutegwa.

Daraja hilo ambalo lilikuwa kiungo Kati ya Kata ya Vighawe na Mpwapwa mjini ambalo Kwa sasa kusombwa na maji.

Kamati ya ulinzi na usalama ikiwa na uongozi wa Tanroad mkoa wa Dodoma ikiongozwa na mkuu wa Wilaya hiyo Bwana Jabir Shekimweri imezungukia maeneo yaliyo athiliwa na kujionea na kuweka mikakati ya njisi ya kurudisha mawasiliano katika Kata hizoo mbili.

Akiongea na wananchi wachache walikuwapo katika eneo hilo Mkuu wa Wilaya hiyo alisema kuwa Kama serikali watahakikisha kuweza kurejesha mawasiliano hayo Kwa haraka iwezekanavyo.

“Natambua kuwa tumeshudia wote mvua zinavyo nyesha kote nchini na kutuletea madhara natambua daraja la kwanza limeondoka na hili sasa ni la pili ndani ya mwezi mmoja hivyo nawasihi wananchi serikali ipo na inalifahamu hili na itafanya kila njia Ili kuweza kurejesha mawasiliano hayo “aliongea

Naye Diwani wa Kata ya Mpwapwa mjini Bwana George Fuime alisema pamoja na daraja hilo kuondoka wanawasiwasi na ubora wa vifaa vilivyo tengenezewa zikiwamo nondo.

“Nina uzoefu katika kazi hizi kwa  muda mrefu lakini pia vifaa vilivyotumika kujengea daraja hili kujea linatupatia wasiwasi  wa kuweza kuondoka  na kusombwa na maji yaani nondo za milimita 6 harafu ziko mbalimbali  kiasi hiki  “alihoji Diwani kata ya Mpwapwa mjini.

Kwa  upande wake  kaimu meneja wa Tanroad mkoa wa Dodoma mwandisi Mwandamizi Bi Salome Kapunda alisema ofisi ya Tanroad mkoa imejipanga kutafuta daraja la muda ili kuweza kurejesha mawasiliano Kwa haraka katika mji wa Mpwapwa.

Akijibia  hoja ya  kuhusu  vifaa vilivyotumika kujengea daraja hili mwandisi Kapunda alisema  kuwa vifaa vilivyotumika ni sahihi kutokana hilo ni daraja la mfuto “ hili  suala  la vifaa kitaalamu halina shida  kilichosababisha hili ni maji mengi” aliongea .

 Mkuu wa wilaya hiyo bwana Jabiri Shekimweri   alisema  makazi ya watu waishio hazina  vighawe  na mjimpya yako hatarini zaidi na  watu lazima wachukue tahadhari mapema kutokana na hali hiyo inaweza kusababisha  maafa .

 “Lakini mpaka sasa tayari baadhi ya kaya zimesha hama  na kwenda sehemu ambayo ni salama  ili kuweza kuokoa maisha yao” aliongea Shekimweri.

 Hata hiyo Shekimweri aliongeza kuwa kwa hatua ilipofikia korongo hilo wilaya kama wilaya haitaweza bali wanaomba nguvu serikali kuu ili kuweza kunusuru hali hiyo, hivyo amewaomba  wadau  wa maendeleo ya mazingira kushirikiana  na wilaya  hiyo kuweza kunusuru  maafa yanayoweza kujitokeza   kutokana na korongo hilo  mjini hapa.