Na Stephen Noel-Mpwapwa.
Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha kote nchini zimeendelea kuathiri miundo mbinu ya barabara na madaraja ambapo Kwa sasa daraja ambalo liko karibu na ofisi za umeme Tanesco kusombwa na maji na kupelekea mji huo kuendelea kutegwa.
Daraja hilo ambalo lilikuwa kiungo Kati ya Kata ya Vighawe na Mpwapwa mjini ambalo Kwa sasa kusombwa na maji.
Kamati ya ulinzi na usalama ikiwa na uongozi wa Tanroad mkoa wa Dodoma ikiongozwa na mkuu wa Wilaya hiyo Bwana Jabir Shekimweri imezungukia maeneo yaliyo athiliwa na kujionea na kuweka mikakati ya njisi ya kurudisha mawasiliano katika Kata hizoo mbili.
Akiongea na wananchi wachache walikuwapo katika eneo hilo Mkuu wa Wilaya hiyo alisema kuwa Kama serikali watahakikisha kuweza kurejesha mawasiliano hayo Kwa haraka iwezekanavyo.
“Natambua kuwa tumeshudia wote mvua zinavyo nyesha kote nchini na kutuletea madhara natambua daraja la kwanza limeondoka na hili sasa ni la pili ndani ya mwezi mmoja hivyo nawasihi wananchi serikali ipo na inalifahamu hili na itafanya kila njia Ili kuweza kurejesha mawasiliano hayo “aliongea
Naye Diwani wa Kata ya Mpwapwa mjini Bwana George Fuime alisema pamoja na daraja hilo kuondoka wanawasiwasi na ubora wa vifaa vilivyo tengenezewa zikiwamo nondo.
“Nina uzoefu katika kazi hizi kwa muda mrefu lakini pia vifaa vilivyotumika kujengea daraja hili kujea linatupatia wasiwasi wa kuweza kuondoka na kusombwa na maji yaani nondo za milimita 6 harafu ziko mbalimbali kiasi hiki “alihoji Diwani kata ya Mpwapwa mjini.
Kwa upande wake kaimu meneja wa Tanroad mkoa wa Dodoma mwandisi Mwandamizi Bi Salome Kapunda alisema ofisi ya Tanroad mkoa imejipanga kutafuta daraja la muda ili kuweza kurejesha mawasiliano Kwa haraka katika mji wa Mpwapwa.
Akijibia hoja ya kuhusu vifaa vilivyotumika kujengea daraja hili mwandisi Kapunda alisema kuwa vifaa vilivyotumika ni sahihi kutokana hilo ni daraja la mfuto “ hili suala la vifaa kitaalamu halina shida kilichosababisha hili ni maji mengi” aliongea .
Mkuu wa wilaya hiyo bwana Jabiri Shekimweri alisema makazi ya watu waishio hazina vighawe na mjimpya yako hatarini zaidi na watu lazima wachukue tahadhari mapema kutokana na hali hiyo inaweza kusababisha maafa .
“Lakini mpaka sasa tayari baadhi ya kaya zimesha hama na kwenda sehemu ambayo ni salama ili kuweza kuokoa maisha yao” aliongea Shekimweri.
Hata hiyo Shekimweri aliongeza kuwa kwa hatua ilipofikia korongo hilo wilaya kama wilaya haitaweza bali wanaomba nguvu serikali kuu ili kuweza kunusuru hali hiyo, hivyo amewaomba wadau wa maendeleo ya mazingira kushirikiana na wilaya hiyo kuweza kunusuru maafa yanayoweza kujitokeza kutokana na korongo hilo mjini hapa.
More Stories
NIDA yawakumbusha wananchi kuchukua vitambulisho vyao
Dkt.Kafumu:Uteuzi wa Rais Samia umezingatia katiba
Kliniki ya sheria bila malipo yazinduliwa Kilimanjaro