
Muonekano wa Kituo cha kupokea Kupoza na kusambaza Umeme kilichohengwa wilayani kilombero Ifakara kinatarajiwa kuzinduliwa Mei 31 na Dkt. Doto Mashaka Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati pamoja na Mhe. Christine Grau, Balozi wa Umoja wa Ulaya.
Kituo hicho kimejengwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa ufadhili wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) ambapo kukamilika kwake kumefanikisha Wilaya ya Kilombero, Ulanga na Malinyi kuwa na umeme wa uhakika.

More Stories
EWURA yatangaza bei ya mafuta
Msajili wa Hazina akutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa EADB
Tanzania mwenyeji wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani