May 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtemvu: Diwani, Mbunge asiyefanya kazi za Ilani afai uongozi

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Dar Es Salaam Abbas Mtemvu, amesema Diwani yoyote wa chama cha Mapinduzi katika Mkoa huo na Mbunge asiyetekeleza Ilani ya chama afai kwa uongozi .

Mwenyekiti wa CCM mkoa Abas Mtemvu, alisema hayo katika mkutano wa hadhara Jimbo la Segerea wa utekekezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Bonnah Ladslaus Kamoli

.”Diwani aliyopo madarakani na Wabunge wao asiyefanya kitu kwake katika utekekezaji wa Ilani ya chama na kuwatumikia Wananchi hawafai kuchaguliwa ” alisema Mtemvu .

Mtemvu amewataka viongozi waliopo madarakani ambao wanatokana na chama CCM kuwatumikia Wananchi katika shughuli za kijamii na kutatua kero kwa utekekezaji wa Ilani ya chama ikiwemo kusimamia miradi ya Maendeleo ambayo imetelekezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Rais Samia Suluhu Hassan. .

Aliwataka vijana ,Wanawake na Watu wenye ulemavu kila Kata kuchangamkia fursa za kiuchumi kwa kuunda vikundi Ili waweze kupata mikopo ya asilimia kumi ambayo aina riba inayotolewa ngazi ya Halmashauri .

Wakati huo huo Mwenyekiti wa CCM mkoa Abbas Mtemvu, alitumia fursa hiyo kutatua kero za Wananchi wa Jimbo la Segerea, Kata ya Bonyokwa na Kinyerezi katika maeneo yaliokosa maji ya Dawasa kwa kuongea na Eng ,Mkuu wa Dawasa Makao makuu na kukili ni kweli maeneo ya Msingwa na Kifuru maji hayafiki kutokana na presha ndogo DAWASA imechukua changamoto hiyo sasa hivi mradi mkubwa wa maji unajengwa wa shilingi bilioni 41 mradi utajengwa Bangulo Hali ya hewa na utasambaza maji maeneo yote mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia Mwezi Agosti mwaka huu mkataba utasainiwa rasmi alisema Eng Mkuu wa Dawasa kwa njia ya simu .

Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli, alisema mkutano huo ni wa Utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM ambapo alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .

Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuwatumikia Watanzania na Jimbo la Segerea kwa ujumla .

Mbunge Bonnah alieleza baadhi ya Barabara zinazojengwa Jimbo la Segerea na Rais ikiwemo Bonyokwa Segerea Tanrods ,Kisukuru Bonyokwa ujenzi umeanza maji chumvi.

Aidha Mbunge Bonnah alisema katika sekta ya Elimu ametekeleza ni Jimbo la pili lenye Miundombinu ya elimu bora na ni Jimbo la nane lenye Wananchi wengi pia Wanaume Jimbo la Segerea wengi Wanawake wachache .

Akizungumzia sekta ya Elimu alisema mwaka 2021 wamepokea bilioni 28 za sekta ya Elimu wamejenga Madarasa na vyoo pia kuna fedha (TAMISEMI ) wanaleta kwa ajili ya kujenga shule nyingine ya kisasaAidha Mbunge Bonnah Kamoli, alisema katika utekekezaji wa Ilani wamejenga kituo cha Afya Segerea ,Kinyerezi ,Mnyamani .

Alisema mvua za El NINO zinatarajia kunyesha Octoba Mwaka huu kama walivyotangaza Mamlaka ya hali ya hewa ametaka mradi wa kuboresha miundo mbinu ya Jiji (DMDP)uwanze haraka Ili kujenga Barabara za ndani za Wananchi wake alisema maendeleo yotote yanataka ushirikiano na Umoja amewataka Wataalam wanaojenga bonde la Msimbazi waanze kujenga Jimbo la Segerea .