Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa Dar es Salaam Abbas Mtemvu, amewataka Umoja wanawake (UWT )kuacha makundi ya uchaguzi badala yake wajipange kuwa wamoja katika kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani 2025.
Mwenyekiti Abbas Mtemvu ,amesema hayo wilayani Ilala katika semina ya UWT ambayo imeandaliwa na Umoja wanawake UWT Wilaya ya Ilala kwa viongozi wa Kata na Matawi kwa ajili ya kuwapatia elimu ya Fedha na mikopo ,Elimu ya uwandishi wa barua ,majukumu ya uongozi na maandalizi ya Uchaguzi .
“Mwaka 2024 chama cha Mapinduzi tutashinda Mitaa yote nawataka umoja wanawake UWT kuacha longo longo na fitina nashangazwa kuona watu wapo katika Makundi wakati Uchaguzi umeisha naomba Wanawake muwe wamoja kujenga chama na Jumuiya “amesema Mtemvu.
Mwenyekiti Mtevu amewataka wanawake wote wenye uwezo kuchukua fomu za kugombea dola katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 katika nafasi ya Ubunge na Udiwani Wanawake Wana uwezo mkubwa pia wanaweza .
Amesema Wanawake Wana uwezo mkubwa wanaweza Mitaa mingi inaongozwa na Wanawake pia wamefanya vizuri katika uongozi wao Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa( MNEC )Simba Juma Gadaf alisema CCM itaendelea kushika dola katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Wabunge ,Rais na Udiwani 2025.
Mwenyekiti wa Umoja wanawake UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa, amewataka UWT Ilala kuwa mkombozi wa Mwanamke wafanye Siasa na uchumi katika kujenga chama na Serikali .
Mwenyekiti Neema amewataka wanawake wa UWT washirikiane na kuhubiri upendo na kujenga chama na Jumuiya zake katika kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Rais 2025.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa Dar es Salaam Nasra Mohamed amewapongeza UWT Wilaya ya Ilala kuandaa semina kwa viongozi wa kata na Matawi Elimu waliopata waende kukisimamia chama na Jumuiya zake.
Mwenyekiti Nasra amewataka wanawake wa UWT changamoto za Kitaifa zilizojitokeza kuisaidia Serikali na kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua