March 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtanzania aula Ujerumani, ni katika tamasha Kimataifa la filamu la Afrika

Na Andrew Chale,timesmajira,online

MTANZANIA mwenye asili ya Zanzibar Muslim Nassor maarufu kama Jazzphaa Jazz anayefanya shughuli zake nchini Ujerumani amechaguliwa kuwa mmoja wa watakaokuwa kwenye tamasha kubwa la Kimataifa la filamu za Afrika, zitakazofanyika Koloni, Ujerumani.

Kwa mujibu wa Jazz, Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi tarehe 16 – 26 September mwaka huu.

“Ninayo furaha ya kuwatangazia nimepata kuchaguliwa kuwa mmoja wa watu ambao watatambulisha filamu na kuongoza maongezi ya filamu Kimataifa katika tamasha la Filamu za Afrika hapa nchini Ujerumani Koloni.” Ameeleza Jazzphaa.

Ambapo amebainisha kuwa, filamu 97 kutoka nchi 25 za Afrika zinatarajiwa kuoneshwa kwenye tamasha hilo.

Ikumbukwe kuwa, Mwaka 2016 mtengenezaji wa Filamu kutoka Tanzania Amil Shivji pia alipata nafasi ya kuchaguliwa kuonyesha Filamu yake ya Aisha.

Aidha, Jazzphaa amewashukuru wadau wote kwa ushirikiano katika harakati zake mbalimbali ikiwemo ya kuongoza shughuli kwenye matamasha makubwa ya Kimataifa ikiwemo tamasha la Kimataifa la Filamu la nchi za Majahazi (ZIFF), Tamasha la Muziki la Sauti za Busara na mengine mengi pindi awapo Visiwani Zanzibar, Tanzania.

“Safari inaendelea. Asanteni wote mlionifanya kuwa na nguvu ya kuamini ninacho kifanya.” Alimalizia Jazzphaa.

Tamasha hilo kwa mwaka huu ni la msimu wa 18 ambapo kila mwaka kimekuwa likipokea filamu mbalimbali kutoka Mataifa yote ya Afrika ambapo majaji uchagua zilizo bora na kuzipitisha.