November 20, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Yas yasherehekea mwaka katika usiku wa utamaduni, ubunifu

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

KAMPUNI Yas Tanzania, imesherehekea “Mwaka wa Viwango” pamoja na washawishi (influencers) na watengeneza maudhui walioshiriki kuunda mwaka huu, katika usiku wenye mandhari ya Kiswahili uliofanyika Mikocheni, ukiwa na muziki wa moja kwa moja na onesho la ngoma ya Kigoma.

Wanamuziki G-nako na Hamadai pamoja na wasanii wengine walioimba wimbo wa kampeni ya “Magifti ya Viwango”, wametumbuiza moja kwa moja mbele ya wageni.

Mwaka huu, Yas imefanya kazi na washawishi 30 na watengeneza maudhui zaidi ya 100 nchi nzima.

Kwa pamoja, wamesimulia hadithi za nchi inayozidi kuunganishwa, kuanzia vichekesho na mtindo wa maisha hadi uwezeshaji wa vijana, ujasiriamali na maisha ya kila siku ya kidijitali.

Sauti zao zilisogeza chapa ya Yas karibu zaidi na jamii inazozihudumia, na kuonyesha jinsi usimulizi wa hadithi za kwetu unavyoweza kuwafikia hadhira mbali zaidi ya mipaka ya Tanzania.

“Watengeneza maudhui ni miongoni mwa wasimulizi wa hadithi wenye nguvu zaidi wa wakati wetu,” amesema Christina Murimi – Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano – Yas Tanzania.

“Mwaka wa Viwango umekuwa kuhusu kuinua viwango katika ubora wa mtandao, katika huduma na katika fursa tunazosaidia kuzifungua. Kufanya kazi na washawishi 30 na watengeneza maudhui zaidi ya 100 kunaonyesha kinachotokea pale chapa na jamii vinapokua pamoja. Usiku wa leo ni njia yetu ya kusema asante, ” ameongeza.

Kwa uoande wake watengeneza maudhui waliohudhuria sherehe hiyo, wamesema ushirikiano huo uliwasukuma kubuni zaidi.

“Kufanya kazi na Yas kwa mwaka mzima kumenipa nguvu. Nimepewa changamoto ya kufikiri nje ya boksi na kutengeneza maudhui yanayoziba pengo kati ya malengo ya kampuni na utamaduni wa Kitanzania,” amesema Willy Nkya.

Kwa kuujenga usiku huo kuzunguka mila za Kiswahili na ngoma ya Kigoma, Yas ilisisitiza kuwa mustakabali wa kidijitali wa Tanzania umejikita katika urithi wake, huku utamaduni ukibaki kiini cha jinsi hadithi zinavyosimuliwa mtandaoni.

Yas imesema, itaendelea kuunga mkono jamii ya wabunifu wa Tanzania kupitia ushirikiano endelevu, msaada kwa watengeneza maudhui na mafunzo.