Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MASHINDANO ya Riadha ya Wanawake yanayojulikana kwa jina la ‘Ladies First’, msimu wa nane, yanatarajiwa kufanyika Novemba 28 hadi 29, mwaka huu, katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Kibaha, mkoani Pwani.
Mashindano hayo yanalenga kutoa fursa kwa wanariadha wa kike kushiriki na kuonesha vipaji vyao katika mchezo wa riadha.
Lakini pia, yakihamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo na kuibua vipaji vipya vitakavyoweza kuiwakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
Msimu huu wa nane unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, ukiwa sehemu ya juhudi za kuendeleza riadha ya wanawake na kupata wanariadha wengi wa kike watakaoweza kujiandaa kuelekea mashindano ya Riadha ya Dunia.
Mashindano ya Ladies First ni sehemu ya juhudi za kukuza na kuendeleza vipaji vya wanariadha wa kike nchini Tanzania.
#@@@#@@@#122111

More Stories
Yas yasherehekea mwaka katika usiku wa utamaduni, ubunifu
Yas yazindua kampeni ‘Magifti Viwango’,zawadi kushindaniwa
Yas, Mixx zaunga mkono Lake Victoria Marathon