April 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtaalamu aeleza Sababu zinazochangia wazee kufia gesti

Na Aveline Kitomary,TimesMajira Online,Dar es Salaam.

HIVI karibu kumekuwa na matukio kadhaa yanayoripotiwa ya wanaume wenye umri mkubwa kufariki katika nyumba za kulala wageni wakati wanapofanya ngono na wasichana.

Mtaalamu wa Saikolojia kutoka Chuo cha Kikatoliki cha Mwenge (MWECAU), Cristian Bwaya ametaja sababu za wanaume mbao umri umeenda kupoteza maisha wakati wanaposhiriki ngono na wasichana.

Akizungumza na Jarida la Majira ya Afya,Bwaya alisema kadri umri unavyozidi kusonga mbele wazee wanatakiwa kubadilisha mifumo ya maisha ikiwemo matumizi ya nguvu na ulaji.

“Kwa kadiri umri unapokuwa unasonga watu wanakuwa na matatizo mbalimbali ikiwemo ya moyo,kisukari na mengine,wazee wengi wanashauri kubadilisha mifumo ya maisha kama ulaji wa aina fulani ya vyakula.

“Wapo wazee wengi wana changamoto za kiafya,ukiacha afya kuna hali ya kupunguza uwezo wa tendo la ndoa,kuna mabadiliko ya kisaikolojia ule uwezo aliokuwa nao ujana unakuwa haupo tena,” alisema.

Alisema kuwa wanaume wengi wanapokuwa na mafanikio hasa ya kifedha wanaona kuwa wanaweza kufanya vitu wasivyoweza kufanya hivyo kama hawana maadili hujiingiza katika mahusiano na wanawake wengi hasa wa umri mdogo.

“Kuwa na mahusiano na wanawake waliozidi umri au wasichana wadogo anaonekana bado anapenda kustarehe lakini wakati mwingine ni changamoto za ndoa anatafuta watu wa kupoteza nao muda anakutana na wanawake wadogo mfano umri wa mtoto wake anakuwa hawezi kumtosheleza.

“Ile kujaribu ‘kuprove’ kuwa anaweza anaingia kwenye mtego wa kutumia dawa za kuongeza nguvu ambapo dawa hizo zinaweza kusababisha magonjwa kama presha na magonjwa mengine unakuta anafia nyumba ya kulala wageni,”alibainisha Bwaya.

Alieleza kuwa wanaume ambao umri wao umeenda na wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali kiafya kuwa na mahusiano na mabinti wadogo ni kujiweka katika hatari.

“Wanaume wanakuwa wamechoka kiafya na kuwa na mahusiano na mabiti wadogo hiyo inawagharimu.

“Kingine kutumia dawa ni shida na wakati mwingine sio dawa utakuta hawaendani na mwenzake hii inaleta changamoto anazindiwa na kupelekwa spidi ambayo haiwezi,”alifafanua Bwaya.

Mwishoo…