December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Msemaji Mkuu wa Serikali ataja mafanikio ya Mkutano wa AGRF

Na David John timesmajira online 

MSEMAJI Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa  amesema kuwa  kufanyika kwa  Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula  (AGRF) hapa nchini ni jambo kubwa na hakuna budi kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani hayo ni matokeo ya dhamira yake kukuza uchumi.

Amesema wageni kama hao wanapokuja hapa nchini kutoka nchi 70  na kunapata wageni zaidi ya 4000 katika mkutano mmoja haiwezi kuwa rahisi kama mipango na jitihada zinazofanywa na viongozi na kwa kushirikiana na wengine hazifanyiki.

Msigwa ameyasema hayo leo Septemba 5, 2023 katika kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere kilichopo Halmashauri ya Jiji la Ilala mkoani Dar es Salaam.

Amesema kuwa Rais Dkt. Samia anafanya kazi kubwa na matokeo yake yanaonekana Sasa” Leo watu hawa waliopo Tanzania wanatumia fedha ambazo pia zinaingia kwa  watanzania lakini muhimu ni kwamba kwa kufanyika mkutano huo hapa nchini kumekuwa na fursa za kunufaika kwa ukaribu zaidi na hata mijadala mbalimbali mifano mingi inatolewa Tanzania, habari nyingi ni za Tanznaia kupitia mkutano huu tu.”Amesema 

Ameongeza kuwa Sasa kama Taifa “Tunayaaambia mataifa mengine Afrika kwamba  Tanzanaia kuna ardhi ya kutosha zaidi hekari milioni 44 zinazofaaa kwenye kilimo nakwamba Tanzania tumeamua kuwekeza kwenye kilimo na kuwasihi wawekezaji kuwekeza kwa kushirikiana na watanzania kuzalisha mazao ya aina mbalimbali.”amesisitiza Msigwa  na kuongeza kuwa

“Kuna mazao kama mbegu za mafuta ,mchele ,mahindi,ngano pamoja na ufugaji  hivyo mkutano huu ni muhimu sana Kwa watanzania na Kwa bahati.nzuri unafanyika wakati wa Serikali yetu inachukua hatua madhubuti za kufanya mageuzi kwenye kilimo .”Amesema 

Pia Msemaji huyo wa Serikali amefafanua kuwa  katika maandalizi ya mkutano wenyewe umewakilisha vyema na wageni wapo huru wanapita mabanda mbalimbali na wanafurahia na kupata nafasi ya kujifunza mambo mbalimbali japo wageni wamekuwa wengi lakini kituo hicho Kina kumbu nyingi na mikutano inaendelea kwenye kumbi hizo.

Akizungumzia eneo la sekta ya habari Msigwa amesema Habari ni Sanaa hivyo lazima waandishi wa Habari wakati mwingine wajuwe  kuwa watu wanataka nini lakini kuna kasumba yakutoa taarifa ambazo wakati mwingine zenye mitazamo furani nakwamba inatakiwa kutoa taarifa na Habari ambazo wananchi wanazitaka na si vinginevyo.

Amesema kuwa mkutano huo ni fursa azmu Kwa wanahabari Kwa kuhakikisha kwamba watanzania wanelewa umuhimu na ukubwa wa mkutano huo na mambo kama hayo hayatokei Kila wakati na Kwa hapa nchini ni mara ya pili kunafanyika Mikutano hiyo.

“Mikutano hiii inafanyika kwa sababu Serikali imechukua hatua madhubuti za kujali kilimo,kuimarisha mifumo ya chakula ambayo ndio ajenda ya mkutano huu kwahiyo waandishi tuchukulie mkutano huu Kwa uzito wake na tufanye uchambuzi .”Amesema Msigwa 

Msigwa amesema kuwa Katika kuona vyombo vya Habari vina umuhimu mkubwa amezitaka taasisi kuona umuhimu wadau kutumia vyombo hivyo ili taarifa mbalimbali ziweze kufika kwa wadau ili wananchi waweze kujua mambo yanayoendelea kupitia mkutano huo na maeneo mengine .