May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Msajili wa Vyama vya wafanyakazi akutana na TRAWU

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kaimu Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri -Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Pendo Berega , amefanya kikao na viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu uliopo katika jengo la PSSSF jijini Dodoma, tarehe 10 Juni, 2022.

Kikao hicho kimejikita Katika kujadili changamoto za kiutendaji za Chama hicho wakati wa utekelezaji wa majukumu yao pamoja na namna bora ya kushirikiana na matawi yao ikiwemo; Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA).

Ofisi ya Msajili wa Vyama Huru vya Wafanyakazi na Waajiri ni moja ya vitengo vilivyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Ofisi hiyo, ilianzishwa mwaka 2000, baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha Sheria ya Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri Na.10 ya Mwaka 1998.

Madhumuni yake ni kuruhusu haki na uhuru kwa wafanyakazi na waajiri kuanzisha na kujiunga na vyama vya wafanyakazi na waajiri kwa hiari yao.