Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
SERIKALI imesema,inatarajia kuanza programu ya kukuza ujuzi kwa vijana mwaka 2024 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 9 zimetengwa kwa ajili ya program hiyo.
Hayo yamesema na Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof . Joyce Ndalichako wakati akizungumza kwenye mahafari ya 40 ya Chuo cha VETA Dodoma .
Prof.Ndalichako amesema kwa mwaka 2024,Programu imelenga kuwafikia vijana 6000 huku akisema lengo la programu hiyo ni kuwawezesha vijana kujiari na kujitegemea kiuchumi na hivyo kuchangia katika pato la Taifa.
“Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 9 kwa ajili ya program ya mafunzo na kukuza ujuzi kwa vijana 6000 itakayoanza Januari 2024.”amesema Prof.Ndalichako
Amesema mafunzo ya ujuzi ni eneo la kipaumbele kwa serikali la kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa kuwawezesha vijana waweze kujiajiri au kuajiriwa na kuondokana na utegemezi kwa familia zao na taifa kwa ujumla.
Katika hatua nyingine Prof.Ndalichako amesema, kupitia mikopo inayotolewa kwenye ngazi za halmashauri serikali itaendelea kutoa kipaumbele kwa vijana ambao wamepata ujuzi.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Prosper Mgaya, amesema mafunzo ya Kukuza Ajira na Ujuzi (E4D) yameleta chachu ya kuleta maendeleo katika chuo hicho.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Frenkly Rwezimula amekitaka VETA kuanzisha program mbalimbali ambazo zitawafikia vijana wengi na zitakazolenga kuongeza thamani kwenye bidhaa mbalimbali
Naye Mshauri wa Mradi wa E4D ,Leah Dotto amesema mafanikio ya Mradi huo ni pamoja na kuwafikia wanafunzi zaidi ya 40000 .
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria