May 2, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mradi Tanga – Pangani kukamilika Agosti

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mradi wa Tanga – Pangani (km 50) unaofadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja (100%), kumekuwa na mvua kubwa za mara kwa mara katika eneo la mradi, mabadiliko ya hali ya hewa hasa uwepo wa mvua nyingi umekuwa ukizuia shughuli za ujenzi kuendelea kama ilivyopangwa, Mkandarasi ameomba nyongeza ya muda ili aweze kukamilisha kazi ambapo kwa sasa Mkandarasi amepewa nyongeza ya muda wa matarajio (Interim Extension of Time )ya miezi mitatu (3) hadi tarehe 24 Agosti 2023.

Eng: Rwekiza ameongeza kuwa ujenzi wa tuta la barabara umekamilika kwa 75%, Magari yameruhusiwa kwenye baadhi ya maeneo kupita  juu ya tuta la barabara mpya inayojengwa kwa kuwa maeneo hayo awali yalikuwa na madaraja madogo ambapo huwa yanazidiwa na maji na kufanya yasipitike, Magari yakisha pita sehemu za madaraja Mapya makubwa hurejea kwenye njia ya mchepuko, na kwamba tahadhari zote zimechukuliwa kuhakikisha hakuna uharibifu kwenye barabara mpya na endapo uharibifu utatokea basi Mkandarasi atarekebisha kwa gharama zake mwenyewe.

Aidha, barabara hiyo ni kiunganishi cha nchi za Kenya na Tanzania upande wa Pwani ya Afrika Mashariki na ikikamilika itachochea ukuaji wa uchumi ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa usafiri, urahisishaji wa kufanya biashara na kuwezesha wananchi kuchangamana kwa urahisi, kuwezesha kufikika kwa urahisi kwenye vituo vya utalii na kuwa kiungo kizuri cha bandari za Dar es salaam, Tanga na Mombasa na kuchochea uchumi wa Bluu.