December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Morogoro yaongoza kwa kumdhamini Rais Magufuli

Na Penina Malundo Timesmajira Online

CHAMA cha Mapindunzi (CCM) Mkoa wa Morogoro, kimeongoza kwa wanachama wengi kumdhamini Rais John Magufuli katika kuwania nafasi ya Urais kwa awamu nyingine kwa kupitia Chama hicho.

Mwenyekiti CCM Mkoa, Innocent Kalogeris amewasilisha takribani Fomu za Wanachama 117,080 kumdhamini Rais leo Mkoani Dodoma alipokuwa akirudisha fomu za kugombea.

Mbali na wadhamini hao waliojitokeza kumdhani Rais Magufuli, pia Mwenyekiti huyo amekabidhi pesa zilizochangwa na wana CCM Mkoa huo, kiasi cha Sh. milioni moja kwa ajili ya kumpa Rais Magufuli.