



Na Mwandishi Wetu,Dodoma
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo na Muhimbili (MOI) imetii agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuendelea kutoa huduma za kibingwa na kibobezi kwenye Maonesho ya Nanenane, Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma, hadi Agosti 10, 2025.
Awali, huduma hizo zilipangwa kuhitimishwa tarehe 8 Agosti 2025, lakini kufuatia agizo la Rais, MOI itaendelea kuhudumia wananchi kwa siku mbili zaidi ili kuhakikisha watu wengi zaidi wananufaika na huduma hizo muhimu

More Stories
UWT yahimizwa kusimamia malezi bora
Uwekezaji wa Michezo wavutia Watalii Tanzania
Mkurugenzi Bonde Rufiji, ahimiza utunzaji vyanzo vya maji