December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mobetto miongoni mwa wanawake 100 wavumbuzi Afrika, atoa shukrani

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MWANAMITINDO mahiri hapa nchini na msanii wa muziki wa Bongo fleva, Hamisa Mobetto ametoa shukrani za dhati baada ya kutajwa kuwa miongoni mwa wanawake 100 wavumbuzi Barani Afrika.

Akitoa shukurani hizo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, Mobetto amesema licha ya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa MobettoStyles lakini siyo yeye peke yake bali walimpandisha ni wateja zake.

“Ni kwa nguvu za Mungu tu. Shukrani za dhati kutajwa mmoja kati ya Watu Mashuhuri wenye Tija katika Wanawake Wavumbuzi 100 Africa.

“Nikiwa kama Mvumbuzi, Muanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa MobettoStyles, ila yote hii sio mimi bali imetokana na Wateja wangu wapendwa na Mashabiki zangu, nyie ndio sababu haswa na nina Deni kubwa kwenu bado. Daima nitakuwa Mtu wa Shukrani, Na Kazi Iendelee,” amesema Mobetto.