December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mobetto awashukuru mashabiki kumuunga mkono

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Mwanamitindo hapa

nchini Hamisa Mobetto ambaye kwa sasa anatamba na wimbo

wake mpya ‘Exwangu remix’, amewashukuru mashabiki zake

kwa kuupokea vyema wimbo huo.

Akitoa shukrani hizo kupitia kwenye Ukurasa wake wa

Instagram Mobetto amesema, amefurahi kuona mashabiki

zake wamempa sapoti kubwa jambo lililochangia kuwa na

Views 500k YouTube ndani ya siku moja.

“Asanteni sana ndugu zangu.Tumefanikwa kuwa na views

500k YouTube ndani ya Siku moja, kwangu ni kitu kikubwa

sana kunisapoti Mimi umemsapoti Senetakilaka na

tunasaidia kutangaza nchi yetu, ona sasa Kenya/Oman/

America/Nigeria/ Kote wanacheza Singeli,” amesema

Mobetto.