Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Moshi
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin babu, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ya kuongoza Watanzania hasa wa mkoa wa Kilimanjaro ambao umepelekewa sh. bilioni 217 kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wake kwa ajili ya maendeleo.
Babu ametoa kauli hiyo leo kwenye Kongamano lililoandaliwa na Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Babu amesema katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia Kilimanjaro imenufaika sana.
“Tumeletewa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali sh. bilioni 217 na zimeenda sekta ya elimu, afya, barabara, maji, kilimo. utalii na uwezeshaji wananchi na ushirika,” alisema RC Babu.
Amesema sekta ya afya peke yake imepelekewa sh. bilioni 42.5 na zimefanyakazi kubwa sana. “Na jana (juzi) tumeletewa sh. bilioni 2.5 kwa ajili ya kumalizia jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Mawenzi,” alisema Babu.
Kwa upande wa sekta ya elimu, amesema walipelekewa sh. bilioni 21 ambazo wamejenga shule mpya za sekondari tisa na walipelekewa sh. bilioni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.
Kwa upande wa Wakala wa Barabara TANROADS mkoa wa Kilimanjaro, Babu alisema mkoa huo umepelekewa sh. bilioni 53 na juzi wamepelewa sh. bilioni 12.5 kwa ajili ya kukarabati uwanja wa ndege wa kilimanjaro. Kwa upande wa maji, alisema zimepelekwa sh. bilioni 14 na miradi inaendelea, kilimo utalii na mazingira nako wanajitaidi.
Amesema ilikukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, mkoa huo wamepokea maelekezo Alisema wameelekezwa kupanda na sasa wanapanda miti ya kutosha.
Kwa upande wa kilimo zimepelekwa sh. bilioni 10 kwa ajili ya mbolea ya ruzuku na kwamba mkoa huo umepewa pikipiki wamepewa 245 kwa ajili ya maofisa ugani kwa ajili ya kuendelea shughuli za kilimo na kwamba mikopo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu inazidi kutolewa kwa kasi kubwa.
Amepongeza juhudi ambazo zinachukuliwa na Serikali kwa hatua za kukuza utawala bora na demokrasia na uwepo wake kwenye kongamano ni kielelezo kwamba wameamua kuwa kitu kimoja.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria