December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini, George Mkuchika akizungumza wakati akipokuwa anawahutubia wananchi wa jimbo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Chikoma wilayani Newala mkoani Mwara juzi. Picha na Anthony Siame.

Mkuchika ahimiza Newala kushiriki uchaguzi oktoba

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Newala Mjini, George Mkuchika amewahimiza wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kupiga kura wakati wa uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika oktoba mwaka huu, Mkuchika alisema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Vijiji vya Mkoma na Imani vilivyopo katika jimbo hilo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jumanne jioni kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mkoma, pia Mkuchika alielezea maendeleo yaliyofanywa  Serikali ya Awamu ya Tano kwa nchi nzima ikiwa ni pamoja na katika Jimbo la Newala Mjini.