Na Mwandishi wetu,Biharamulo.
HIFADHI ya Taifa ya Burigi -Chato imetumia kiasi cha sh bilioni 3.3 kuimarisha Miundombinu ndani ya hifadhi ili kuvutia watalii kutembelea hifadhi hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2019.
Akizungumza na waandishi wa habari,Mkuu wa hifadhi hiyo, Kamishina Msaidizi Ismaili Omari amesema Maboresho ya Miundombinu ya hifadhi ni jitihada zinazofanywa na Shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA )kuboresha miundo mbinu mbalimbali ndani ya hifadhi hiyo kufikia malengo ya serikali Tanzania kupokea milioni 5 ifikapo mwaka 2025
Mhifadhi Omar amesema barabara zenye urefu wa kilomita 97.5 pamoja na madaraja na vivuko yamejengwa hadi sasa umekamilika ujenzi wa kambi za Utalii pamoja na makazi ya bei nafuu ya watalii ndani ya hifadhi hiyo.
“Tumejenga barabara zinapitika wakati wote lakini pia madaraja na kuna minara ya Mawasiliano ambayo imejengwa ndani ya hifadhi tofauti na miaka ya nyuma,hivi sasa Watalii wanaweza kuwasilisha”amesema
Afisa utalii hifadhi ya Burigi- Chato ,Aldo Mduge amesema upekee wa hifadhi hiyo ni uwepo wa ndege aina ya Domo kiatu (African Shoebill) maziwa yanayo zunguka hifadhi wanyama wengi na ndege aina 400.
Akizungumzia makazi ya ndani ya hifadhi, Kaimu mkuu idara ya utalii hifadhi hiyo, Emmanuel Nyundo hiyo alisema uwekezaji walio ufanya ikiwemo kujenga kambi ya wageni ya kudumu huku akiwakaribisha wageni kuwekeza Burigi kwani kuna maeneo mazuri.
Hifadhi hii ina kilomita za mraba 4707 katika wilaya za Biharamulo,Chato,Karagwe ,Ngara na Muleba,ipo katika mikoa ya Kagera na Geita.
More Stories
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais