November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Miti kupandikizwa ndani ya maabara

Na Grace Gurisha,TimesMajira Online

KATIBU wa Kongano Bunifu la Mwani Zanzibar (ZaSCI), Rajab Ali Ameir amesema ushirikiano na msaada wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) wapo mbioni kuanzisha kupandikiza miti ndani ya maabara.

Ameir amesema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea banda la Costech kwenye maonesho ya 46 ya sabasaba, ambapo tume hiyo ndiyo imewafadhili kuja kwenye maonesho hayo, Dar es Salaam.

“Costech imeweza kutupa ujasili kwa sababu tumezungumza na taasisi nyingi za utafiti hadi kufikia hatua ya kutaka kutengeneza maabara za kupandikiza miti ndani ya maabara,”amesema Ameir

Katibu huyo, amesema kupitia kongano hilo wameungana na watafiti mbalimbali na kumeweza kuongeza thamani ya zao la mwani kwa kutengeneza bidha tofauti
zitokanazo na mwani.

Amesema wanatengeneza mafuta nywele, stimini ya nywele, losheni, mafuta ya mgando, sabuni mbalimbali za kuogea na unga mwani unaotumika katika lishe ili kumpa mtoto nguvu au virutubisho kwa sababu mwani ni mmea wenye vitamini.

“Mwani unasaidia mgongwa wa goita, sukari, matatizo ya presha, kansa kwa sababu ni mmea unasaidia kuongeza kinga ya mwili kutokana na virutubisho vyake,”

” Sifa kuu ya mwani ukiweka katika kitu kinafanya na kujikusanya kwa pamoja na ndiyo maana mwani unatumika katika viwanda vya vyakula mfano viwanda vya kutengeneza ice cream, chocolate ili iwe ngumu,”amesema

Amesema mwani unalimwa na kusafirishwa nje, zamani walikuwa wakiwasilisha asilimia 100, lakini kwa sasa ndani ya Zanzibar angalau kupitia kongano hili la mwani kwa kushirikiana na Costech angalau asilimia mbili wameweza salifu kwa kutoa bidhaa tofauti na asilimia 98 ndiyo wanasafirisha nje.

“Hili kongano bunifu lilitokana na kuona zile tabu na shida walizokuwa wakikutana nazo wakina mama kule Zanzibar wakulima wa mwani, kwa hiyo tukaanzisha kwa ajili ya kuwasaidia wakina mama kutatua shida zao haswa ilikuwa ni bei ya mwani,”amesema

“Msaada wa Costech umetuunganisha sisi na wanasayansi na watafiti, sisi tunafanya kazi na watafiti tunafanya na Serikali, na Wizara tofauti. Tunaishukuru Costech kwa sababu mwani hadi kujua unaliwa na kuwekwa kwenye juisi kule Zanzibar na kwa sasa hivi ni kwa Tanzania nzima tangu mwaka 2005 bado tupo nao,”amesema