May 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Miradi ya maji safi,usafi wa mazingira ya SBL yawawezesha wanawake

Mkuu wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Rachel Kassanda akimkabidhi cheti mmoja wa wanufaika wa mafunzo ya ujasiriamali na utunzaji wa vyanzo vya maji kwa wanawake yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Serengeti Breweries yaliyofanyika tarehe 5 Mwezi March mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza, Rachel Kassanda, akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Mwanamke Duniani na mafunzo ya WASH kwa wanawake wa kijiji cha Kabila.
Wakazi wa kijiji cha Kabila wilayani Magu mkoani Mwanza, wakiwa na vyeti vyao baaada ya kukabidhi walipomaliza mafunzo ya ujasiriamali na utunzaji wa vyanzo vya maji kwa wanawake yaliyodhamini na Kampuni ya Serengeti Breweries mwishoni mwa mwezi Februari, Tukio hili la kukabidhi vyeti lilihudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Magu, Rose Kassanda.

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online MWANZA

KAMPUNI ya bia ya Serengeti imeendeleza juhudi zake za kuimarisha upatikanaji wa huduma za maji, usafi wa mazingira, na usafi (WASH) kwa wanawake sambamba na mipango ya serikali ya kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo ya vijijini.

Katika dhamira yake ya kutimiza lengo hili, SBL imedumisha miradi yake jumuishi nchini ili kuwapa watu maji safi na salama. SBL imetoa ufadhili wa huduma nyingine muhimu ya WASH inayolenga hasa kuwawezesha wanawake na wasichana katika wilaya ya Magu mkoani Mwanza, katika mradi mkubwa unaojulikana kama Mradi wa Maji wa Kabila.

Mradi huu unafanywa kwa ushirikiano na Africa Community Advancement Initiative (AFRIcai), NGO inayojihusisha na afya, elimu, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika jamii mbalimbali za Kitanzania. Ushirikiano huu wa kimkakati unalenga kuondoa uhaba wa maji kwa kuwapatia maji safi na salama wananchi 11,927 katika vitongoji vitano vya Ilambu, Mlimani, Igogo, Shuleni na Majengo.

Aidha, kwa kutambua nafasi muhimu ya wanawake katika kuhakikisha uendelevu wa miradi hiyo, SBL na AFRICAi waliendesha programu maalumu ya mafunzo ya siku mbili ambapo wanawake ishirini na tano (25) waliwezeshwa ujuzi na maarifa muhimu katika masuala mbalimbali ya shughuli za WASH, ujasiriamali, usimamizi wa fedha, usafi  wa kimasoko, wa mazingira, na kukuza jitihada za usafi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bonanza la WASH, Rispa Hatibu, Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL, alisisitiza umuhimu wake: ‘tunaandaa tukio hili ili kukuza uwiano wa kijamii na ushirikiano wa jamii, na kusisitiza umuhimu wa uwekezaji wa WASH katika eneo hili. Zaidi ya hayo, tukio hili linaangazia jukumu muhimu linalofanywa na vikundi vya wanawake katika kuhakikisha umiliki wa mradi na uendelevu’.

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Magu, Rachel Kassanda, alisisitiza umuhimu wa kuulinda mradi huo ili kujikimu kimaisha na kuhakikisha uendelevu wa vizazi vijavyo. Alipongeza juhudi za ushirikiano za SBL na serikali, akisema kuwa ni faida kwa sekta zote mbili. Hasa, alisisitiza umuhimu wa kuwawezesha wanawake katika maeneo ya vijijini kupitia mipango kama hiyo.

Katika kila jumuiya ambapo SBL inatekeleza miradi ya WASH, kamati huwa zinaundwa zenye uwakilishi sawa kutoka kwa wanaume na wanawake, ikikuza fursa za maamuzi jumuishi na uendelevu wa muda mrefu. Zaidi ya hayo, midahalo ya jumuiya hufanyika ili kushughulikia kanuni za kijamii na kitamaduni zinazozuia ujumusishwaji wa wanawake kwa WASH huku pia zikiwashirikisha wanaume na wavulana katika mchakato huo.