Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online MWANZA
KAMPUNI ya bia ya Serengeti imeendeleza juhudi zake za kuimarisha upatikanaji wa huduma za maji, usafi wa mazingira, na usafi (WASH) kwa wanawake sambamba na mipango ya serikali ya kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo ya vijijini.
Katika dhamira yake ya kutimiza lengo hili, SBL imedumisha miradi yake jumuishi nchini ili kuwapa watu maji safi na salama. SBL imetoa ufadhili wa huduma nyingine muhimu ya WASH inayolenga hasa kuwawezesha wanawake na wasichana katika wilaya ya Magu mkoani Mwanza, katika mradi mkubwa unaojulikana kama Mradi wa Maji wa Kabila.
Mradi huu unafanywa kwa ushirikiano na Africa Community Advancement Initiative (AFRIcai), NGO inayojihusisha na afya, elimu, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika jamii mbalimbali za Kitanzania. Ushirikiano huu wa kimkakati unalenga kuondoa uhaba wa maji kwa kuwapatia maji safi na salama wananchi 11,927 katika vitongoji vitano vya Ilambu, Mlimani, Igogo, Shuleni na Majengo.
Aidha, kwa kutambua nafasi muhimu ya wanawake katika kuhakikisha uendelevu wa miradi hiyo, SBL na AFRICAi waliendesha programu maalumu ya mafunzo ya siku mbili ambapo wanawake ishirini na tano (25) waliwezeshwa ujuzi na maarifa muhimu katika masuala mbalimbali ya shughuli za WASH, ujasiriamali, usimamizi wa fedha, usafi wa kimasoko, wa mazingira, na kukuza jitihada za usafi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bonanza la WASH, Rispa Hatibu, Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL, alisisitiza umuhimu wake: ‘tunaandaa tukio hili ili kukuza uwiano wa kijamii na ushirikiano wa jamii, na kusisitiza umuhimu wa uwekezaji wa WASH katika eneo hili. Zaidi ya hayo, tukio hili linaangazia jukumu muhimu linalofanywa na vikundi vya wanawake katika kuhakikisha umiliki wa mradi na uendelevu’.
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Magu, Rachel Kassanda, alisisitiza umuhimu wa kuulinda mradi huo ili kujikimu kimaisha na kuhakikisha uendelevu wa vizazi vijavyo. Alipongeza juhudi za ushirikiano za SBL na serikali, akisema kuwa ni faida kwa sekta zote mbili. Hasa, alisisitiza umuhimu wa kuwawezesha wanawake katika maeneo ya vijijini kupitia mipango kama hiyo.
Katika kila jumuiya ambapo SBL inatekeleza miradi ya WASH, kamati huwa zinaundwa zenye uwakilishi sawa kutoka kwa wanaume na wanawake, ikikuza fursa za maamuzi jumuishi na uendelevu wa muda mrefu. Zaidi ya hayo, midahalo ya jumuiya hufanyika ili kushughulikia kanuni za kijamii na kitamaduni zinazozuia ujumusishwaji wa wanawake kwa WASH huku pia zikiwashirikisha wanaume na wavulana katika mchakato huo.
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango