May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Milioni 212 zatolewa kwaajili ya Vifaa Tiba Makongolosi

Na Esther Macha, TimesmajiraOnline,Chunya

WANANCHI wa Mamlaka ya mji mdogo Makongolosi wilayani Chunya mkoani Mbeya wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kupelekewa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 212 ikiwa ni awamu ya kwanza.

Na kutegemea kupokea vifaa vingine kwa awamu ya pili vitakavyo kamilisha shilingi milioni 300 zilizotolewa na Rais Samia kwaajili ya vifaa tiba katika kituo hicho.

Pongezi hizo zimetolewa katika kituo cha afya cha Makongolosi kata ya Bwawani wakati wananchi walipofika kushuhudia makabidhiano ya vifaa hivyo kutoka Bohari ya Dawa(MSD)ambavyo vitarahisha huduma nyingi ikiwemo upasuaji ambapo awali walikuwa wakizifuata huduma hizo hospitali ya wilaya.

Mmoja wa wananchi wa Mji wa Makongolosi wilayani humo Hilda Fande na Amosi Mwazembe, wakazi wa kata ya Bwawani mamlaka ya mji mdogo Makongolosi kwa niaba ya wananchi waliojitokeza kushuhudia mapokezi ya vifaa tiba katika kituo cha afya Makongolosi wamefurahi kwa kusogezewa huduma za afya hususani vifaa vya upasuaji pamoja na jokofu la kuhifadhia miili ya wapendwa wao walio tangulia mbele za haki.

Wamesema kuwa kipindi cha nyuma iliwalazimu kuifuata huduma hiyo katika hospitali ya Wilaya kitu ambacho kilikuwa ni changamoto kubwa kwao.

“Tunashukuru sana mama yetu kutusogezea huduma sisi wakinamama tulikuwa tunahangaika sana kipindi cha nyuma tulikuwa tukiondokewa na wapendwa wetu tunalazimika kupeleka Hospitali ya Wilaya ya Chunya,”amesema Fande

Naye Mwazembe amesema kuwa walikuwa na changamoto kubwa kipindi cha nyuma kwan8 walikuwa na huduma ya zahanati tu lakini kwasasa wanakituo cha afya na leo wameletewa vifaa tiba kama jokofu la kuhifadhia miili ya wapendwa wao wanapowatoka hivyo alimshukuru tunamshukuru Rais Samia kwa kuwajali wananchi wake.

Diwani wa kata ya Bwawani,Sailon Pashila amemshukuru Rais Samia kwa kuwaletea vifaa tiba na kusema kuwa wananchi hawata pata adha ya kwenda mbali tena kupata huduma za afya hususani upasuaji na huduma zingine.

“Sasa nawaambia wananchi waondoe shaka Changamoto za kwenda kufuata huduma katika hospitali ya wilaya ya Chunya na Mbeya sasa labda kwa huduma za dharua pale itakapobidi kwani serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi chini ya Rais Samia Suluhu Hassani inawajali wananchi wake kwa sasa tunaomba serikali ituongeze na Watalam wa afya ili huduma ziweze kutolewa kwa wakati” amesema Mpashila

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Chunya,Linus Mwanitega Mtendaji wa Mamlaka ya Mji mdogo Makongolosi amesema kuwa vifaa tiba vilivyopokelewa vinaenda kujibu matatizo ya wananchi ikiwa ni pamoja na huduma za upasuaji pamoja na huduma ya kuhifadhi wapendwa wao kwa kuletewa jokofu la kuhifadhia miili ya wafu.

“Tumepokea vifaa muhimu kwasababu vinakwenda kujibu matatizo na hoja mbalimbali za utoaji wa huduma kwa wananchi wetu kwakweli haikuwa laisi lakini kwa juhudi za rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassani ameweza kutuletea vifaa tiba vyenye thamani ya million 212 na tunategemea kupokea vifaa vingine ambavyo vitakamisha million 300 hivyo utoaji wa huduma kiyuo cha afya Makongososi utakuwa wakisasa tofauti na ilivyokuwa awali”amesema Mwanitega

Awali akitoa taarifa ya upokeaji wa vifaa hivyo Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mfamasia wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya, Edward Tengulaga amesema kuwa vifaa vilivyopokelewa vyenye thamani ya mil.212 ni pamoja na Vitanda 70 vya kulaza wagonjwa, magodoro 70, Kitanda cha upasuaji , Utra sound pamoja na vifaa vingine.

“Tumepokea vifaa hivi vyenye thamani ya million 212 kwa awamu ya kwanza lakini tunategemea kupokea vifaa vingine kabla ya tarehe 15 na tunategemea kuanza kutoa huduma za upasuaji kuanzia tarehe 15 Machi na utoaji wa huduma nyingine unaendelea kama kawaida kwa wananchi wa Mamlaka ya mji mdogo Makongolosi” amesema Tengulaga