Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Sherehe ya wakulima na maonesho ya nanenane kilele kilikuwa Agousti 8,2022 huku
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA) Kanda ya Ziwa ikishika nafasi ya tatu katika kundi la mamlaka ya usimamizi na udhibiti.
Pamoja na utoaji huduma bora kwa wananchi waliofika katika banda lao kwenye maonesho ya nanenane Kanda ya Ziwa Magharibi yaliyofanyika katika uwanja wa Nyamhongolo wilayani Ilemela mkoani Mwanza kuanzia Agousti 1-8,2022.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha maonesho hayo Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa George Mhina, ameeleza kuwa
waliwapa taarifa zote sahihi na muhimu watu wote waliofika na kutembelea katika banda lao ili waweze kupata tenda na kama kuna kampuni wataisajili kwanza kwenye kanzi data yao.
Mhina ameeleza kuwa wataalam wao wenye ueledi waliweza kujibu maswali yalioulizwa na wateja katika banda lao bila kuchoka na kwa usahihi.
Ambapo amefafanua na kueleza kuwa watu wengi walikuwa wanauliza maswali mbalimbali ambayo wataalamu wa EWURA Kanda hiyo waliweza kuwajibu ikiwa ni pamoja na suala la maji.
“Wananchi wengi walihitaji kufahamu kuhusu suala la maji kwa Mwanza na maeneo mengine Kanda ya ziwa ambapo walipata ufafanuzi wa kutosha kuhusu miradi mbalimbali inayoendelea kutekeleza ambayo itakuwa suluhisho la changamoto ya upatikanaji wa maji,”ameeleza Mhina.
Pia ameeleza kuwa wananchi walihitaji kufahamu fursa zinazopatikana katika mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) linalotoka Hoima nchini Uganda kwenda Chongoleani Tanga nchini hapa.
“Wananchi walitaka kufahamu mradi huo umefikia wapi,ni nini wanaweza kufaidika na ni fursa zipi wanaweza kupata ambapo wataalamu wetu waliwapatia majibu na ufafanuzi sahihi,”.
Sanjari na hayo Mhina ameeleza kuwa walihitaji kufahamu kuhusu utaratibu wa ujenzi wa vituo vya mafuta vya gharama nafuu maeneo ya vijijini.
Ambapo alifafanunua kuwa wamejikita katika kutoa elimu na wametengeneza kanuni ndogo ambazo ni rafiki hivyo mtu akiwa na milioni 40 mpaka 50 anaweza kujenga kituo cha vijijini na wananchi wakapata huduma ya mafuta kwa bei iliyopangwa na Ewura ambayo ni bora na salama kwa watumiaji.
Katibu wa Kamati ndogo ya upimaji wa tathmini ya maonesho ya nanenane na sherehe za wakulima Kanda ya Ziwa Magharibi Robert Samwel, wametoa zawadi ya fedha taslimu, kombe pamoja na vyeti kwa washiriki waliokuwa chachu kwa wengine katika kufikisha kauli mbiu ya mwaka huu inayosema ‘agenda 10/30 kilimo ni biashara shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo, mifugo na uvuvi’.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam