November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhandisi Mahundi: Serikali kuanza kuchukua hatua waharibifu vyanzo vya maji nchini

Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Morogoro

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesema kuwa serikali haitavumilia uharibifu wa vyanzo vya maji ambao umekuwa ukifanyika katika maeneo mbali mbali nchini na kwamba  serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan imeelekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maji na kwamba Wizara haitavumilia uharibifu huo.

Imeelezwa kuwa tayari  unaofanywa  uchunguzi umeanza  kufanyika  na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Mhandisi Mahundi ametoa onyo hilo katika mwendelezo wa ziara yake mkoani Morogoro ambapo amesikitishwa na watu wasiojullikana kuharibu miundombinu ya mradi huo unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 3.

Aidha Naibu Waziri huyo  ameaonya wananchi wa kijiji cha waliong’oa mabango yaliyowekwa na kuharibu alama za mipaka kwa ajili ya utunzaji wa chanzo cha maji katika vijiji vya Chiwachiwa na Kisegese Wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro.

“Eneo hili la mto Lwipa lipo chini ya usimamizi wa bodi ya maji bonde la mto Rufiji ambao waliweka bikon mia mbili kuzunguka eneo hilo ikiwa ni ishara ya ukomo wa shughuli za kibinadamu lakini kundi la watu wasiofahamika wameng’oa bikoni 180”amesema  Mhandisi Mahundi .

Kufuatia uharibifu huo Naibu waziri huyo aliwataka wananchi kuilinda miundo mbinu ya maji kwani serikali inatumia fedha nyingi ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

Kwa upande wake meneja wa Wakala wa maji vijijini RUWASA Wilaya ya Kilombero ,Flolence Mlelwa amesema kwa sasa serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa tanki la lita laki mbili na nusu na mradi unatarajiwa kuhudumia vijiji vyote Kata ya Mbingu na Igima ambapo vituo thelathini vikitarajiwa kujengwa.

Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godfrey Kunambi ameishukuru serikali kwa kutatua changamoto iliyokuwa inawakabili wananchi wake ya upatikanaji wa maji safi na salama Jimboni kwake.