May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mha.Mahundi ataka watendaji kusimamia utekelezaji miradi ya maji

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online,Pwani

Watendaji wa sekta ya maji wilayani Mafia wametakiwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji ili ikamilike kwa wakati na wananchi wapate huduma hiyo kwa uhakika.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi alipofanya ziara ya kikazi wilayani Mafia kwa kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maji ya Jibondo, Kilindoni pamoja na kuzindua mradi wa maji wa Jimbo(Kidika).

Mhandisi Mahundi akiwa katika miradi hiyo amewataka watendaji wa sekta ya maji wilayani Mafia kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama na yenye kutosheleza.

Pia ametoa maelekezo kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi kwenye Wilaya hiyo kuwa kuhakikisha inakamilika kwa wakati na iendane na ubora wake.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Mafia Zephania Sumaye ameishukru serikali kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Mafia ikiwemo miradi ya maji ya Chunguruma-Ndagoni, Kilindoni, kanga, Kibada pamoja na mradi wa maji wa Jibondo.