January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mgombea ubunge Jimbo la Manyoni Mashariki Dkt.Pius Chaya akipita mitaani kusalimia wananchi mara baada ya kurejesha fomu za kuwania nafasi hiyo.

Mgombea Ubunge Manyoni ataja vipaumbele vyake

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Manyoni

MGOMBEA ubunge jimbo la Manyoni Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Pius Chaya amesema miongoni mwa vipaumbele vyake pindi akichaguliwa na wananchi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo ni kujenga hosteli za watoto wa kike ili kupunguza mimba kwa wasichana shuleni.

Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wilayani humo ,Dkt.Chaya amesema matukio ya wasichana kupata mimba na kukatisha masomo yao yanasababishwa na ukosefu wa hosteli lakini pia kukosa mazingira mazuri ya kusomea wawapo nyumbani.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimvo la Manyoni Mashariki Charles Fusi akipokea fomu za mgombea ubunge wa jimbo hilo Dkt.Pius Chaya

“Mimba mashuleni na ukosefu wa hosteli bado ni tatizo,hili nitalifanyia kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali”amesema Dkt.Chaya

“  Hapa ni mjini tunahitaji kuwa na barabara za lami lakini tuna barabara moja kubwa sana ya kutoka Manyoni kwenda Sanza-Heka-Chikola

hadi Dodoma ,mipango niliyonayo ni pamoja na kuunganisha barabara hiyo ya wilaya ya Manyoni na Mkoa wa Dodoma.”alisema Dkt.Chaya