Na Heri Shaaban
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Angelina Malembeka, ametoa ahadi ya kuchangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya msingi Fahari ambayo inatarajia kuanza ujenzi wake hivi karibuni .
Mbunge Malembeka aliyasema katika mahafali ya awali ya Watoto ya Fahari Day Care ambapo alisema naunga mkono juhudi za serikali kwa upande wa elimu kuwekeza watoto wa Taifa letu waweze kupata elimu .
“Ninachangia mifuko 100 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Mpya ya Fahari Day Care wameamua kuwekeza katika Elimu sasa hivi wanajenga Shule ya msingi tuwaunge mkono” alisema Malembeka.
Malembeka alipongeza Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo kuwekeza katika sekta ya elimu kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Aliagiza uongozi wa Shule ya Fahari kupima eneo hilo la Shule mapema kwa ajili ya kuondoa migogoro ya ardhi wavamizi wasivamie Wakaleta migogoro ya ardhi .
Aidha aliwakumbusha Fahari Day Care kupanda miti eneo la Shule ya Msingi katika juhudi za kutunza mazingira kuifadhi vyanzo vya maji
Wakati huo huo Mbunge Malembeka amewakumbusha Wazazi kulipa ada kwa wakati kwa ajili ya shule kujiendesha na kulipa wafanyakazi .
Alisema jambo la Fahari ni jambo letu na fahari yetu hivyo akuna budi kushirikiana pamoja katika kuwekeza katika sekta ya Elimu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fahari Day Car Center alisema kituo kilianzishwa 2014 ni moja ya mradi uliopo Fahari Tuamke Maendeleo walipata usajili 2016 kwa dhumuni la kuisaidia jamii kwa kutoa huduma bora yenye malezi mema kwa watoto kwa kuzingatia utamaduni wa kitanzania.
Neema akielezea mafanikio ya Fahari Tuamke Maendeleo alisema Fahari imefanikiwa kupata eneo kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi kata ya Msongola eneo la Kiboga kwa sasa wapo katika mchakato wa michoro.
Alisema mikakati ya Fahari kuanza ujenzi wa shule ya Msingi itakayojulikana FAHARI ELITE ambayo itakuwa na Shule ya Msingi na shule ya Awali .
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa