January 19, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Utekelezaji wa miradi kata ya Mikocheni

Na Mwandishi wetu, TimesMjira Online

Kwa kipindi kifupi cha uongozi wa awamu ya sita chini ya Mh Rais Samia Suluhu Hassan mambo mengi yamefanyika na yanaendelea kufanyika maeneo mbalimbali ya nchi ya Tanzania ambayo yanaleta mabadiliko ya haraka kuelekea Tanzania ya uchumi wa kati wa juu.


Kuanzia miradi mikubwa hadi midogo ambayo imebadili sehemu kubwa ya sura ya Tanzania, tunaona ujenzi wa madaraja makubwa na madogo,hospitali,zahanati na vituo vya afya maeneo mengi huduma hii imefika,ujenzi wa barabara za juu na chini,reli ya umeme(SGR),uboreshwaji wa safari za anga ikiwemo ukarabati wa vituo vya ndege na ununuzi wa ndege sambamba na mipango miji kwa kujenga barabara za mitaa kwa kiwango kulingana na mahitaji ya eneo husika.


Miongoni mwa maeneo ambayo miradi iliahidiwa na viongozi kuanzia madiwani hata wabunge ni Kata ya Mikocheni ambapo wananchi waliahidiwa mambo mbalimbali baadhi yamekamilika na mengine
yakiendelea kutekelezwa kwa weledi wa hali ya juu .


Wananchi wa kata ya mikocheni wamemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan na wasidizi wake kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali inayopatikana katika kata yao chini ya usimamizi mzuri wa Mh Diwani Eng Zenzely Hussein Iddy ambae anasimami utekelezaji wa miradi ndani ya kata na kuhakikisha
inakamilika bila kasoro yeyote.


Wakizungumza na vyombo vya habari wananchi mbalimbali ambao wameguswa na miradi hiyo wamesema pamoja na kumshukuru Rais pia wanamshukuru Waziri wa TAMISEMI Mh Ummy Mwalimu na wanampongeza diwani wa kata hiyo Eng Zenzely Hussen Iddy kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo ambayo imetekelezwa na mingine
inaendelea kutekelezwa katika kata yao.


Ndani ya Kata ya Mikocheni kuna jumla ya miradi nane ambayo ilikuwa kwenye utekelezaji uliyokamilika ni mmoja na inayoendelea kufanyiwa kazi ni miradi saba sambamaba na hiyo miradi mitatu ipo hatua za
mwishoni kukamilika imefikia 90%.


Ujenzi wa barabara ya Regent ya urefu wa km0.64 imekamilika kwa kiwango cha lami iliyokuwa ikijengwa na TARURA imeghalimu zaidi ya Milioni 676.


Vilevile TARURA inaendelea na ujenzi wa barabara kwenye kata hiyo ikiwemo barabara ya Chwako yenye urefu wa km0.6 kwa kiwango cha lami,barabara ya Warioba ya urefu wa km0.78 kwa kiwango cha zege, na barabara ya Migombani ya urefu wa km0.25 kwa kiwango cha lami zote hizi zitakamilika ndani ya miezi sita.


Barabara ya Chato ipo katika mpango wa matengenezo imechukuliwa na TANROAD pia ujenzi wa barabara kuanzia Chama stendi kwenda Marwa Bar inaenda kutokea Chwako na kuanzai Chwako kwenda
Gezaulole inaenda kutokea Sabato church na barabara ya Lukuledi,Msikiti,Kiko street,School road pamoja na Foundation Street mapendekezo yamewasilishwa TARURA kwaajili ya utekelezwaji wake.


Mtendaji Kata ya Mikocheni amesema endapo barabara hizo zitajengwa zitapunguza adha ambayo wanaipata wananchi wa Mikocheni hasa wakati wa mvua kwani barabara hizo huwa hazipitiki zinajaa maji,pia ni
kero kwa wananchi wa karibu na barabara hizo .


Sanjari na hayo katika kata ya Mikocheni kuna mradi wa ukarabati na ujenzi unaoendelea katika shule za msingi na sekondari,ujenzi wa maabara tatu katika shule ya sekondari Mikocheni ambao unagharimu
zaidi ya Shilingi milioni 235 iliyotolewa na Manispaa ya Kinondoni kwa mwaka wa fedha 2020/2021.


Pia kuna ujenzi wa madarasa matano na ofisi moja katika shule ya masingi Mikocheni ambao unagharimu zaidi ya kiasi cha Shilingi milioni 83 chanzo cha mapato ni manispaa kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pia ukarabati unaendelea wa vyumba vitatu vya madarasa vimeezekwa na kupigwa plasta.


Aidha kuna ujenzi wa madarasa manne ya ghorofa shule ya sekondarin Mikocheni ambao unaghalimu zaidi ya Shilingi milioni 198 iliyotolewa na Manispaa kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ujenzi unaendelea pamoja
na ujenzi wa madarasa manne ya chini ambayo chanzo chake serikali kuu mradi wa UVIKO uliogharimu shilingi milioni 80 ujenzi wake umefikia asilimia tisini uweze kukamilika.


Hamisi Malela ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni akizungumza kwa niaba ya wanafunzi na walimu walioguswa na mradi huo amesema anamshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu pia amempongeza diwani Eng Nzenzely Hussein
Iddy kwa usimamizi mzuri wa mradi huo ambao utaleta mabadiliko katika ufaulu kabla ya kuwa na maabara walikuwa wanatumia vyumba vya madarasa kwaajili ya kufundishia na wanafunzi walikuwa wanafaulu masomo ya sayansi.


Pia amesema ujenzi huo wa madarsa utaongeza ufanisi wa kazi na wanafuzni kuelewa zaidi endapo watakuwa wachache madarasani ujenzi huo wa madarsa ya ghorofa na manne ya chini mradi wa UVIKO
umesaidia sana shuleni hapo.


Hata hivyo Mkandarasi anaesimamia ujenzi huo Eng Angel Michese alisema ujenzi upo katika hatua nzuri na mafundi wapo eneo la kazi mpaka kufikia mwezi wa kwanza majengo yote yataaanza kutumika
kuanzia maabara,madarasa ya ghorofa na madarasa ya UVIKO.


Vilevile kuna mpango wa ujenzi wa zahanati ya kata kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo vifaa vimepatikana muda wowowte kuanzia sasa ujenzi utaanza,kusafisha mto fedha mikocheni na msasani kwa
gharama zaidi ya shilingi milioni6,ujenzi wa choo machinga mwenge utagharimu zaidi ya milioni 20,uchimbaji wa visima kumi na nne Mikocheni A kumi na moja ,darajani visima vitano na uwezeshwaji wa
vikundi mbalimbali, ambavyo vimesajiliwa ni vikundi tisini na vilivyopatiwa mkopo ni sabini na moja.