Na Joyce Kasiki,TimesMajira,Online
MBUNGE wa Makete Festo Sanga(CCM) amewaasa wabunge wenzake kufanya siasa za vitendo katika kuwaletea wananchi maendeleo badala ya siasa za mdomoni.
Sanga amesema hayo jana mkoani Dodoma katika viwanja vya Bunge wakati akiongea na TimesMajira ,amesema kuwa Bunge la sasa ni la kazi na siyo la ndiyo mzee kama wengine wanavyodhani.
“Wote ni mashuhuda,Rais Dkt.John Magufuli amekuwa na ‘speed’ kubwa katika utendaji wake,na sisi wabunge tunatakiwa kwenda na speed ya Rais ,
” Hatutakiwi kuwa na siasa za maneno,tunatakiwa kuzungumza pamoja na kutenda,wananchi wanatakiwa kupata maendeleo kupitia sisi wawakilishi wao.” Amesema Sanga na ameongeza kuwa
“Hilo siyo bunge la ndiyo mzee , siyo kitu kizuri kukaa bungeni kama bubu ,lazima tufanye kazi kwa kasi kubwa .”
Akizungumzia kuhusu jimbo la Makete amesema,jimbo hilo linakabiliwa na changamoto kubwa ya barabara ya kutoka Makete kwenda Mbeya .
“Hilo ni miongoni mwa jambo nitakalolifanyia jitihada kuhakikisha tunapata barabara ya kiwango cha lami kutoka Makete kwenda Mbeya ili kurahisisha usafiri kwa wananchi.” Amesema Sanga
Pia amesema atashughulikia changamoto za zahanati ,Elimu,maji pamoja na michezo.
“Tuna changamoto ya zahanati,lakini ipo ambayo inahitaji kumaliziwa nitafanya hivyo,pia katika suala la Elimu tunatamani kutokomeza ‘zero’ katika jimbo letu hivyo tutaweka mikakati ya nini cha kufanya ili kulifanikisha.” Amesema
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu