May 4, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Jimbo la Konde ajiuzulu,CCM yasikitishwa

Na Mwandishi wetu,timesmajira,online

CHAMA cha Cha Mapinduzi CCM, kimepokea kwa masikitiko barua ya kujiuzulu kwa Mbunge Mteule wa CCM Jimbo la Konde, Sheha Mpemba Faki Leo Agosti 2,2021.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,Itikadi na Uenezi CCM,Shaka Hamdu Shaka amesema katika barua yake, Sheha Mpemba Faki ameeleza kwamba amefikia uamuzi huo kutokana na changamoto za kifamilia, jambo ambalo Chama hakina uwezo wa kumzuia, hasa ikizingatiwa kwamba ni haki yake ya msingi kama ilivyo kwa haki ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ndani ya CCM.

Amesema Chama chao kinawaomba wanachama wote kuwa watulivu katika kipindi hiki wakati tukisubiri taratibu nyingine.