*Yumo mganga wa kienyeji, mfanyakazi wa mochwari
Na Ashura Jumapili TimesMajira online Bukoba,
Jeshi la Polisi Mkoani Kagera linawashilikiwa watu wawili akiwemo mfanyakazi wa chumba cha kuhifadhi maiti(mochwari) hospitali ya Bwawa wilayani Mbozi mkoani Songwe pamoja na mganga wa kienyeji, kwa tuhuma za kupatikana na viungo vinavyodhaniwa kuwa vya binadamu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda,amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Kelvin Mdollo( 42 )Mnyiha ambaye ni mganga wa kienyeji na mkazi wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe pamoja na Randani Mlomo mfanyakazi wa chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Vwawa iliyopo wilayani Mbozi mkoani Songwe.
Chatanda,amesema, awali Juni 17,2025,walimkata Mdollo,akiwa na viungo vinavyodhaniwa kuwa vya binadamu,ambavyo ni mfupa mmoja wa taya inayowezekana kuwa ni ya binadamu, kipande cha moyo wa binadamu,kipande cha sehemu ya siri ya mwanamke na kipande cha kondo la nyuma la tumbo la uzazi la mwanamke.
Pia mtuhumiwa huyo alikamatwa na vipande viwili vya ngozi iliyokaushwa idhaniwayo kuwa ya nyoka aina ya chatu,ngozi moja ya nyoka wa kawaida,pembe mbili za mnyama wa porini,vipande vitatu vya mifupa ambayo bado haijatambulika kama ni ya mnyama au binadamu,ambavyo alikuwa akivitumia katika shughuli za uganga wa jadi na kupiga ramli chonganishi katika nyumba ya kulala wageni inayojulikana kama Standard iliyopo Kata ya Kibeta Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Amesema, baada ya mtuhumiwa wa kwanza ambaye ni mganga kuhojiwa na polisi alimtaja Randani Mlomo ( 64 ) mfanyakazi wa hospitali ya Vwawa chumba cha kuhifadhia maiti iliyopo Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe,kwa madai kuwa ndiye aliyempatia viungo hivyo.
Ambapo amesema ndipo jitihada zilifanyika haraka ambazo zilifanikisha kumkamata Mlomo na kysafirisha hadi mkoani Kagera,hivyo wanaendelea na mahojiano na watuhumiwa hao ili kubaini mtandao mzima unaojihusisha na matukio ya mauaji,ukataji wa viungo vya binadamu,uporaji pamoja na wanaojihusisha na kazi za uganga wa tiba asili bila kuwa na vibali ikiwemo wanaopiga ramli chonganishi ili waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.
Hata hivyo ametoa wito kwa wananch kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kuhusu uhalifu na wahalifu huku akionya watu wote wanaojihusisha na shughuli za uganga wa jadi bila vibali kuacha mara moja akisisitiza kuwa hatua zitachukuliwa kwa watakaokamatwa.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako