January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbaroni kwa kumlawiti mtoto miaka minne

Na Mwandishi wetu,timesmajira,Online

JESHI la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia mtu mmoja mwenye umri wa miaka 16 kwa madai ya kumlawiti mtoto wa miaka 4 na kusababisha kifo.

Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, ACP Muliro Muliro amesema jana kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 10, 2021 majira ya saa tatu asubuhi , Chamanzi Mbande Wilaya ya Temeke.

Amesema uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo unafanyika na hatua za kisheria wakati wa uchunguzi zitazingatiwa  ili itendeke pande zote mbili.