January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkazi wa mji wa Malia uliopo Kisiwa cha Crete nchini Ugiriki akijaribu kuondoa matope yaliyochanganyikana na mchanga baada ya kuzingira magari kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi mjini humo. (Picha na Reuters).

Matukio yaliyosisimua katika picha

Mwanamke akipatiwa vipimo vya virusi vya Corona (COVID-19) kupitia mpango wa kuwafikia watu majumbani mjini Ammerschwihr uliopo Mashariki mwa Ufaransa juzi. (Picha na AP).
Mwanaume aliyeonekana akiwasiliana kwa simu huku akiwa juu ya ngamia kati kati ya vyombo vya moto katika moja ya barabara zenye pilika nyingi mjini New Delhi, India juzi. (Picha na AFP).
Rais wa Baraza la Jumuiya ya Ulaya, Charles Michel (kushoto) na Kansela wa Austria, Sebastian Kurz (kulia) wakitoa ishara ya heshima kwa watu waliouawa kupitia shambulio la kigaidi hivi karibuni mjini Vienna, Austria. (Picha na AP).
Wanaume waliokutwa wakiokoa mapipa ambayo yalikuwa sokoni na kubebwa na mafuriko katika eneo la Toyos nchini Honduras hivi karibuni. (Picha na Reuters).