December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Binti raia wa Syria akiwapa maua askari wa Jeshi la Marekani baada ya kutua eneo la Kaskazini Mashariki mwa Syria karibu na mji wa al-Malikiyah (Derik) kwa ajili ya kufaya doria katika miji inayokaliwa na Wakurdish karibu na mpaka wa Uturuki juzi. Vita vinavyoendelea nchini humo vimesababisha maelfu kupoteza maisha, makazi na wengine kuyakimbia makazi yao. (Picha na AFP).

Matukio mbalimbali ulimwenguni (picha)

Mvuvi akielekea kuvua samaki kama alivyokutwa katika Mto Yamuna mjini New Delhi, India juzi. (Picha na AFP).
Picha iliyopigwa Juni 8, mwaka huu ikionyesha maafisa wa Kikosi cha Uokoaji huku mmoja wao akiwa amembeba mtoto waliyemuokoa katika maji ya mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha mjini Qingyuan uliopo Kusini mwa Jimbo la Guangdong nchini China. (Picha na AFP).
Afisa usalama akifanya ukaguzi kuhakikisha kila abiria ndani ya treni amekaa kwa kuacha nafasi ikiwa ni muongozo wa Wizara ya Afya kujiadhari na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) katika stesheni ya Bogor mjini Bogor, Indonesia jana. (Picha na EPA-EFE).
Watu wakisubiria kupimwa virusi vya Corona (Covid-19) katika moja ya vituo vilivyotengwa na Serikali mjini Marina Bay, Singapore juzi. Serikali hiyo imeweka vituo vya namna hiyo nchini kote kuhakikisha kila mtu anaenda kupimwa kwa hiyari ili kuliweka Taifa salama. (Picha na JASON QUAH/ST).