November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkazi wa Sangam mjini Saraswati, Allahabad nchini India akifanya mazoezi ya Yoga kama alivyokutwa Juni 20, mwaka huu. Umoja wa Mataifa umeidhinisha kila ifikapo Juni 21 ya mwaka kuwa Siku ya Kimataifa ya Yoga, mazoezi ambayo yanaleta afya ya mwili na ya akili pamoja na amani baina ya watu huku wataalam wakisisitiza yana faida nyingi zaidi hususani kipindi hiki cha Corona. (Picha na AFP).

Matukio mbalimbali duniani katika picha

Mhudumu wa afya akichukua vipimo vya COVID-19 kutoka kwa mwanamke mmoja juzi, kupitia dirisha dogo mjini New Delhi, India ikiwa ni muendelezo wa hatua za Serikali kuhakikisha inawapima raia wake ili kufahamu walioambukizwa kwa hatua zaidi za kitatibu. (Picha na AFP).
Kima wakivuta mkia wa paka juzi katika moja ya jengo lililopo mjini Lopburi uliopo zaidi ya kilomita 155 Kaskazini mwa Bangkok, Thailand. Mji huo unasifika kwa idadi kubwa ya kima ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya utalii ndani ya miaka mitatu watalii zaidi ya 6,000 wamekuwa wakifika kwenda kuwaona. (Picha na AFP).
Bibi Agustina Canamero (81) na mume wake Pascual Perez (84) wakibusiana kupitia kitenganishi maalum cha plastiki ambacho kinaondoa uwezekano wa viungo kugusana, lengo likiwa ni kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) mjini Barcelona, Hispania juzi. (Picha na AP).
Msusi wa kike akimsuka mteja katika moja ya saluni za kike zilizopo mjini Bogota, Colombia juzi huku wakiwa wamechukua tahadhari zote dhidi ya virusi vya corona (COVID-19). Ugonjwa wa corona upo, hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha tunachukua tahadhari kila wakati. (Picha na AFP).