Na mwandishi wetu, TimesMajira Online
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (Mb) amewataka wananchi wa eneo la Ubaruku Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya kuendelea kutunza na kuhifadhi mazingira ili waendelee kufaidika na uwepo wa mvua na hali ya hewa nzuri.
Ameyasema hayo leo katika Ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta Mkoani Mbeya.
“Tunapoharibu maeneo ya Hifadhi na mazingira tunasababisha mvua zisije” amesisitiza.
Naibu Waziri Masanja amefafanua kuwa wananchi wamevamia maeneo ya Hifadhi na kufanya uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji akitolea mfano wa uvamizi katika Mto Ruaha.
Amewaasa wananchi kuacha uvamizi katika maeneo ya hifadhi ili kuondokana na uharibifu wa vyanzo vya maji, ukataji miti na uchomaji mkaa na hatimaye kurithisha vizazi vijavyo.
More Stories
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari