December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Masache aomba serikali kuboresha mawasiliano  jimboni kwake 

Na Mwandishi wetu ,Timesmajira Online,Dodoma

MBUNGE wa jimbo la Lupa wilayani Chunya Mkoani Mbeya , Masache Kasaka ameiomba serikali kuboresha mawasiliano ya mtandao wa simu  katika vijiji  vya Shoga,upendo pamoja na Sipa kutokana na changamoto hiyo kuwepo kwa muda mrefu .

Akijibu swali la nyongeza  la  Mbunge wa Lupa ,Waziri wa Habari  mawasiliano na  Teknolojia, Mhe. Nape Nnauye alisema kuwa mwaka huu wa fedha wametenga minala mingi  kidogo lakini kwa maana eneo maalum  anakotoka Mbunge huyo kuwa na shughuli za kiuchumi zilizopo katika maeneo hayo watazipa kipaumbele  cha peke yake .

Hata hivyo Mhe. Nnauye amesema kama katika orodha walizotoa wakati wa bajeti hizo kata na maeneo yaliyotajwa  hayamo basi nao wataingizwa kwenye  orodha yale maeneo maalum kwasababu ya shughuli nyingi za kiuchumi kufanyika kwenye maeneo hayo .

Aidha Mh. Nnauye  amesema kuwa serikali ipo tayari kusaidia kushirikiana ujenzi wa uchumi wa kidigitali ili uweze kuingia uchumi wa jumla .