December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Markdone Village yazitaka klabu Ligi kuu kujituma kufikia malengo

Na Mwandishi Wetu,Dodoma

KLABU zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara zikiwemo Simba na Yanga zimetakiwa kujituma na kufanya maandalizi mazuri kabla ya mchezo wowote ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kupata ushindi na kufikia malengo.

Kauli hiyo imetolewa jana na Meneja wa kijiji cha michezo cha Mark Done kilichopo jijini Dodoma, Joram Lemanya wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya eneo lao la kisasa la kufanyia mazoezi (Gym).

Lemanya amesema klabu hizo zinapofika Dodoma basi eneo la kufanya maandalizi yao kabla ya mchezo ni Mark Done Village kutokana na vifaa vingi vya kisasa na eneo kubwa.

“Kwa klabu zetu za ligi kuu na klabu nyingine, hapa ni eno sahihi la maandalizi yao kuelekea kwenye michezo ya wanapokuwa huku Dodoma, tuna vifaa vya kutosha na eneo kubwa la kuweza kuwahudumia wachezaji,” amesema Lemanya na kuendelea,

“Naziomba klabu zilete timu zao kwa ajili ya kuweka kambi Mark Done village kila wanapokuwa na uhitaji huo, lakini pia tuna eneo la viwanja hapa jirani ambavyo wanaweza kutumia kufanya mazoezi au kucheza mechi za kirafiki,” amesema Lemanya.

Amesema kwa upande wa timu ya Dodoma Jiji, alisema wanapaswa kutumia eneo hilo kwa ajili ya maandalizi ya mechi mbalimbali za ligi Kuu dhidi ya timu nyingine wanazotarajia kukutana nazo.

Amesema Dodoma jiji inapokuwa na mechi katika uwanja wao wa Jamhuri Dodoma,wanapaswa kutumia Markdon Village kama sehemu maeneo yao ya kufanya mazoezi ya viungo kwa wachezaji.