Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Butiama
WATU mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kushiriki misa ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere iliyofanyika jana katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria, Parokia ya Butiama Jimbo la Musoma.
Misa hiyo imefanyika leo na kuongozwa na Padri Medard Chegele. Miongoni mwa waliohudhuria misa hiyo ni mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere pamoja na viongozi wa Serikali.
Viongozi hao ni pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula ambaye alikuwa mkuu wa wilaya wa kwanza wakati Wilaya ya Butiama inaanzishwa.
Mwalimu Nyerere alifariki mwaka 1999 wakati akipatiwa matibabu nchini Uingereza na kuzikwa kijijini kwao Butihama.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
27 kulipwa kifuta jasho Nkasi
Mwakilishi Mkazi wa UN nchini awasilisha hati