May 13, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Aboubakar Kunenge,akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)jana jijini humo.

RC Kunenge awataka wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya Mvua zinazoendelea kunyesha.

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Aboubakar Kunenge amewataka wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya mvua zinazoendelea kunyesha kwa kuhakikisha wanafuatilia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya hewa TMA ili kujikinga na athari za Mafuriko.

Pia ametoa maelekezo kwa TARURA, TANROAD, DAWASA, REA na TANESCO kuhakikisha wanaendelea kukarabati na kurejesha miundombinu yote iliyoathiriwa na mvua.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari,RC Kunenge amesema mamlaka hizo zinatakiwa kuhakikisha zinarejesha huduma kama awali.

.

Aidha RC Kunenge ametoa pole kufuatia vifo vya watu 12 vilivyojitokeza kutokana na mvua ya juzi ambapo amesema mbali na vifo hivyo pia zaidi ya nyumba 800 ziliathiriwa na mvua na kusababisha kero kwa wananchi.

Pamoja na hayo RC Kunenge ameeleza kuwa Kamati za maafa na vikosi vyote vinaendelea kuzunguka maeneo mbalimbali ya jiji hilo ili kukabiliana na madhara yoyote yanayoweza kutokea.

RC Kunenge ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kutupa taka kwenye mito na Mifereji kwakuwa ndio chanzo Cha mitaro kuziba na kusababisha Mafuriko.