March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makonda:Tekelezeni miradi ya maendeleo hata kama kuna tofauti za kisiasa

Na Queen Lema,Timesmajiraonline,Arusha

MKUU wa mkoa wa Arusha amewataka wanasiasa wote wa mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa wanajijengea tabia ya kupeleka maendeleo mbele kwa wananachi wote bila kubagua na  hata kama wanapingana kwa hoja mbalimbali kwani Kwa kutosimamia ipasavyo utekelezaji wa miradi utasababisha kuendelea kukithiri kwa umaskini

Endapo kama kutakuwa na ubaguzi wa kisiasa miradi mbalimbali ambayo imelengwa kutekelezwa na serikali haitaweza kutekelezwa ipasavyo

Makonda amesema hayo jana kwenye hafla fupi ya uitaji wa saini mikataba miwili ya soko la machinga ,pamoja ujenzi  wa uwanja wa mpira Ambao unatarajia kuanza

Makonda amesema kuwa ni vibaya Sana Kwa wanasiasa kuacha kutekelezwa miradi kwaajili ya matakwa Yao Jambo ambalo linachangia sana kuchelewesha maendeo ya wananchi

“Siasa lazima iwepo lakini tofauti za kisiasa zisitufanye tuache kuchochea maendeleo mfano kuna huu mradi.wa soko serikali ilishatoa ela yote toka 2021 lakini haukufanikiwa na hili limefanikiwa leo kuweza kutokea kwa sababu nimesimama ipasavyo naomba sana hili lisijitokeze tena serikali inapoleta fedha inalenga wote aichagua kuwa wewe upo kambi ipi na ipi”aliongeza Makonda

Aliendelea kwa kusema kuwa Kwa mkoa wa Arusha kwa sasa Agenda kubwa ni maendeleo kwa kuwa Arusha ni miongoni mwa Mikoa ambayo inavutia sana kwenye sekta ya uchumi lakini hata utalii.

“Natamani sana kuona kila MTU ananufaika na wageni ambao wanaokuja Arusha na watanufaika tu endapo kama kutakuwa na uwiano mzuri Kati ya mtendaji wa Serikali lakini pia mwanachi nataka kila MTU asimame kwenye sehemu yake”aliongeza Makonda.

Katika hatua nyingine alisema kuwa nao wananchi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanafuatilia miradi mbalimbali ambayo imesainiwa na endapo kama mkandarasi ataonesha kusuasua basi watoe taarifa mara moja.

“Arusha kulikuwa na tabia ya kusaini mikataba kwa kificho kikubwa lakini Mimi nimekuja na hii Mimi Mambo yote hadharani ili wananchi waweze kujua na kutambua kuwa kulikuwa na mradi na wao sasa wataweza kuyafutilia kwa ukaribu sana “aliongeza

Naye mmoja wa wazubuni waliweza kushinda kwenye zabuni  ya ujenzi wa soko la machinga  ambao ni kampuni ya Suma Jkt construction Ltd walisema kuwa watahakikisha wamemaliza mradi huo ndani ya muda muafaka

Luteni Kanali Daudi Zengo alisema kuwa pamoja na kuwa wameshinda zabuni hiyo watafanya kwa uimara mkubwa sana kwa kuwa wao wanatekeleza shuguli mbalimbali za miradi

Luteni Kanali Zengo alisema kuwa Jiji la Arusha wamewaamini kwenye katika mradi huo na wao watahakikisha kuwa wanakuwa wanatekeleza mradi huo vyema

“Suma Jkt ni kampuni ya kizalendo na itafanya kazi kwa uzalendo mkubwa sana na kwa mradi huu tunatarajia kumaliza hata kabla ya wakati ili wananchi waweze kunufaika”aliongeza