January 27, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Maisha ya kuiga huharibu mahusiano ya wasichana wengi.

Na Aveline Kitomary,TimesMajira online,Dar es Salaam

KUMEKUWA na hali ya kuvunjika  kwa mahusiano mara kwa huku kukiwa  na sababu mbalimbali kwa wahusika.

Kuvunjia kwa mahusiano huonesha utofauti na msimamo wa tabia  za wahusika walioko katika mahusino.

Mara nyingi malengo ya mahusiano ni kufikia hatua Fulani nzuri lakini pale yanapoishia njiani kila kitu huharibika na kuishia hapo.

Mtaalamu wa masuala ya  Saikolojia, Sadaka Gandhi  ameeleza ni kwanini wasichana wengi kwa sasa wanashindwa kukaa katika mahusiano ikilinganishwa na zamani.

Miongoni mwasababu  alizoainisha Msaikolojia huyo ni wasichana wengi wa sasa kupenda kuiga maisha ya wengine huku wakiwa hawajui hao watu wanauwezo gani .

“Wasichana wanapenda kuishi maisha ya kuiga au kuigiza  na  wanajidanya ili waonekane wanaishi maisha ya juu kumbe sio maisha yao halisi.

“Kingine Wasichana wameamua kupoteza thamani yako kwa kutotulia katika mahusiano  kwa kukubali kwa kila mwanaume anayemtongoza au kuwa katika mahusiano zaidi ya moja kwa lengo la kupata anayoyaihitaji,”amesema Sadaka.

Amesema kuwa thamani ya msichana haitoki kwa mwanaume  ila kwa kuitengeneza  mwenyewe kwa kujiamini,kujithamini  na ufata mfumo mzuri unaofaa wa maisha.

“Kuamini kuwa bila mwanaume huwezi kuishi wakati sio kweli unaweza kuijiongezea thamani kwa kujiamini na kufanya kazi zako kwa bidii ukilenga kujitegemea na sio kufanya wanaume kuwa vitega uchumi,”amesisitiza Sadaka.