Na Mwandishi Wetu
RAIS John Magufuli amemteua Dkt. Zainab Chaula kuwa Katibu Mkuu wa Mawasiliano.
Kabla ya uteuzi huo, Dkt.Chaula alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na amechukua nafasi iliyoachwa na Dkt. Maria Sasabo ambaye amestaafu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ilieleza kwamba Rais Magufuli amemteua Prof. Mabula Mchembe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Kabla ya uteuzi huo, Prof. Mchembe alikuwa Msaidizi wa Rais katika masuala ya afya. Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Abel Makubi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.
Kabla ya uteuzi huo, Prof. Abel Makubi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando na amechukua nafasi iliyoachwa na Prof. Mohamed Kambi ambaye amestaafu. Kwa mujibu wa taarifa hiyo uteuzi wa viongozi hao umeanza jana.

More Stories
Wagonjwa 500 wafanyiwa upasuaji wa nyonga na goti MNH-Moganzila
Mgejwa:Nishati Safi ya Kupikia ni fursa ya kiuchumi
Tanzania kujenga Chuo Kikuu cha Usafirishaji cha Kanda