Na Esther Macha,Timesmajira,Online, Mbeya
IMEELEZWA kuwa magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa yakiongoza kuondoa maisha ya wananchi na kwamba kitendo cha wananchi kujitokeza kupima kutasaidia serikali kupunguza gharama za matibabu .
Miongoni mwa magonjwa ambayo yamekuwa na ongezeko ni Kisukari,Moyo,Ini,figo shinikizo la juu la damu,Kansa na matatizo mengine.
Kauli hiyo imetolewa Mei 3,2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya Dkt.Godlove Mbwanji wakati wa maadhimisho ya wiki ya watalaamu wa maabara pamoja na miaka 10 baada ya kupata Ithibati ya kimataifa ya maabara ya hospitali hiyo.
“Tuendelee kuwatia moyo wananchi kuendelea kujenga utaratibu wa kupima kujua afya zao lakini pia waendelee kufuata ushauri wa wataalamu kwenye masuala mazima ya ulaji wa vyakula, mazoezi na mambo mengine yanayohusu afya zetu wote.
“Tunafahamu afya yako ni ndio mtaji wako,na ni mojawapo ya utajiri wa kila binadamu ukiwa na afya nzuri unaweza kupanga mipango yako yote ikawa salama na ikaenda kwa utaratibu hivyo wananchi mliojitokeza kupima afya zenu ni nzuri endeleeni na desturi hii kuwa tabia ya kupima mapema”amesema Dkt.Mbwanji.
Naye Naibu Msajili wa Bodi ya Maabara binafsi Wizara ya afya,Naima Mkingule amesema magonjwa yasiyoambukiza hapa nchini ni asilimia 74 ikiwemo kisukari ,Moyo,ambayo yamekuwa yakisabisha vifo.
Aidha Mkingule amesema kuhusu Tiba utalii inayotolewa hospitalini hapo amezitaka Hospitali zilizopo mipakani ikiwemo hospitali ya Rufaa kanda inayohudumia mikoa saba ya Nyanda za juu kusini pamoja na nchi jirani za Malawi,Zambia ,Congo iboreshe utoaji wa huduma za tiba utalii.
“Wananchi kutumia maabara zaidi za Ithibati ili kuweza kutoa huduma bora na majibu bora ambayo mteja anaweza kuhudumiwa lakini pia anaweza kuondoka na majibu yake kwa kwenda kuhudumiwa kwa kutumia nchi za jirani zinazozunguka hospitali hiyo,”amesema.
Hata hivyo Mkingule amesema kuwa Maabara ya hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya ilipata Ithibati Mei ,2014 na kuwa hapa nchini Maabara zilizopata Ithibati ni nyingi zipo maabara za serikali na maabara binafsi ambazo ni 30 na kwamba mpango wa serikali kuhakikisaha wanaongeza Ithibati za kimataifa ili idadi iweze kuongozeka maabara zinazopima kwa kutoa majibu yanayoaminika na mkakati wa serikali kuhakikisha maabara zote ngazi ya kituo cha afya kwenda juu zitapata Ithibati ambayo imekuwa ikisaidia kuboresha huduma za afya hasa magonjwa yasiyoambukiza .
“Tunafamu sote nchini kuwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza yamekuwa mengi idadi imepanda kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba imezidi magonjwa yanayoambukizwa na vimelea kwa kusema hilo ningeomba jamii ijenge tabia ya kupima vipimo ili kuweza kuzitatua changamoto ambazo zinatokana na magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa ni kikwazo na kusumbua “amesema Naibu Msajili wa Bodi ya Maabara .
Akizungumzia kuhusu kundi linaloathiriwa zaidi na magonjwa yasiyoambukiza Mkingule amesema kuwa mwanzoni walijua ni wazee lakini kwa sasa ni kundi la vijana na rika la kati nao wamekuwa miongoni hasa magonjwa ya moyo , Sukari imekuwa changamoto kubwa hivyo ni vema kuchukua tahadhari mapema.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mbeya , Beno Malisa amesema kuwa uwepo wa hospitali hiyo kwa gharama zote ambazo serikali imeweka ni nia njema kuhakisha wananchi wake wanakuwa na afya njema na faida ya serikali yao wanaiona na manufaa yake.
“Niwaombe wataalamu wetu wa Maabara kuwa na wazalendo kwani matibabu bora yananza na vipimo bora kama kuna roho ya hospitali eneo la kwanza ni hilo kwakuwa hii ni miaka 10, sasa naamini mtaendelea mpaka 20 na zaidi ya hapo na naamini hospitali hii itaendelea kuhudumia wananchi kwa viwango stahiki na kutoa majibu stahiki kama ilivyozoeleka kwa miaka 10 sasa lakini tuendelee kutoa huduma zenu kwa uzalendo,nimekuwa nikipokea malalamiko mbali mbali lakini kwa hospitali hii ya kanda sijawahi kusikia malalamiko yeyote hii inamaana linaloonekana linamalizwa haraka”amesema Mkuu huyo wa wilaya ya Mbeya Beno Malisa.
Isack Nyangi ni Afisa Ubora wa Maabara Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya amesema lengo la kuwa na Ithibati ya kimataifa kwa Maabara ni kukuza ustawi wa wagonjwa na kuhakikisha huduma zinazotolewa ni toshelezi kwa wagonjwa na watumiaji wengine wa huduma za maabara.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi